Uchunguzi wa kibobezi na matibabu ya mapafu na mfumo wa hewa

WATAALAM WA MAGONJWA YA NDANI WAJENGEWA UWEZO MUHIMBILI

Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani pamoja na Hospitali ya Yashoda Hyderabad ya nchini India imefanya kongamo maalum la kuwajengea uwezo wataalam wa magonjwa ya ndani juu ya namna kufanya uchunguzi wa kibobezi na matibabu ya mapafu na mfumo wa hewa.

Akifungua kongamono hilo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MNH Dkt. John Rwegasha amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa njia ya nadharia na vitendo ambapo yatajikita zaidi katika kutambua magonjwa yanayoweza kuathiri mfumo wa hewa namna ya kutumia darubini kufanya uchunguzi na kutibu magonjwa hayo.

“Wataalam hawa watakuwa na uwezo wa kutumia darubini kuchunguza na na kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani, kifua kikuu kilichojificha pamoja na kutoa vivimbe vinavyoweza kujitokeza katika njia ya mfumo wa hewa”,amesema Dkt. Rwegasha.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji MNH,na Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Dkt. Mwanaada Kilima amesema ajenda kuu ya chama chao ni kusaidia kuimairisha huduma za afya na kufanya maboresho kwa kuwajengea uwezo wataalam wa afya nchini.

“Kama ambavyo Muhimbili inafanya uchunguzi na kutibu magonjwa ya mapafu basi tungetamani kuona hospitali zingine nchini zikitoa huduma hizi kwa ufanisi zaidi.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi kutoka Hospitali ya Yashoda Hyderabad, Muhimbili pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) ambapo yamehudhuriwa na waatalam kutoka hospitali mbalimbali ikiwemo na Muhimbili, Mnazi Mmoja , Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, KCMC, Kibong’oto pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!