Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake



 UGONJWA WA KISONONO

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na Bacteria ambaye kwa kitaalam hujulikana kama Neisseria gonorrhoeae na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Ugonjwa huu wa zinaa hushambulia na kuathiri zaidi maeneo ya mwili yenye joto Pamoja na Unyevu unyevu kama vile;

  •  Kwenye urethra au mrija ambao huvuta mkojo kutoka kwenye kibofu
  • Kwenye macho
  •  Eneo la Kooni
  • Ukeni
  • kwenye Uume
  •  Kwenye njia ya haja kubwa(anus)
  • Kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke ikiwemo Kwenye Kizazi,Mirija ya Uzazi, Pamoja na Mlango wa kizazi yaani cervix n.k

UGONJWA WA KISONONO HUSAMBAAJE AU KUAMBUKIZWA?

Ugonjwa huu husambazwa kwa Njia ya Kujamiiana,

Kufanya Mapenzi kwa njia ya Mdomo,Sehemu ya haja kubwa au Ukeni yaani oral, anal, or vaginal sex.

Kutumia kondomu au njia nyingine ya kizuizi unaposhiriki tendo la ndoa kunaweza kusaidia sana kupunguza uwezekano wako wa kusambaza au kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono,

Kumbuka tu matumizi ya njia hizi hayataondoa kabisa hatari ya wewe kupata magonjwa kama haya, hasa ikiwa hutumii kwa Usahihi,

Unaweza kutumia Njia kama Condom na bado ukapata Kisonono(Gono) endapo hukutumia kwa Usahihi wake.

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO);

Kumbuka; Ugonjwa huu wa kisonono kwa asilimia kubwa ni vigumu mwanamke kuonyesha dalili za moja kwa moja hata kama ameambukizwa. Lakini kama akionyesha dalili basi baadhi ya dalili kama hizi hapa chini huweza kutokea.

MIONGONI MWA DALILI AMBAZO HUWEZA KUJIONYESHA KWA MWANAMKE NI PAMOJA NA;

– Mwanamke kupatwa na tatizo la maumivu makali wakati wa kufanya mapenzi

– Mwanamke kutokwa na maji maji ukeni ambayo yana harufu sana

– Mwanamke kutokwa na ute ute ambayo umechanganyika na usaha ukeni

– Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa

– Kupatwa na shida ya blid mara mbili ndani ya mwezi mmoja

– Kupatwa na maumivu makali ya tumbo

– Joto la mwili kupanda au kuwa na homa

– Kuvimba kwenye eneo la mashavu ya uke 

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

– Kutokwa na usaha sehemu za Siri

– Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

– Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

– Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

– Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

– Joto la mwili kupanda au kuwa na homa

MADHARA YA UGONJWA WA KISONONO

je kisonono kinaweza kusababisha matatizo gani?

(1) Ikiwa wewe ni Mwanamke, una nafasi kubwa ya kukumbwa na matatizo ya muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kisonono kama hukupata Tiba ukapona,

Magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama vile kisonono na Chlamydia yanaweza kuleta athari kwenye njia ya uzazi na kuathiri maeneo mbali mbali ikiwemo Kizazi chenyewe(Uterus), mirija ya uzazi Pamoja na ovaries.

Hii inaweza kusababisha matatizo mengine kama vile maambukizi ya bacteria kwenye via vya Uzazi vya Mwanamke yaani pelvic inflammatory (PID),

PID inaweza kusababisha maumivu makali, ya muda mrefu na uharibifu wa viungo vya uzazi.

– Kuziba au kupata kovu kwenye mirija ya uzazi,

Na hii huweza kuleta madhara mengine kama vile;

  • kufanya iwe vigumu zaidi Kwa mwanamke kupata mimba
  • kusababisha tatizo la mimba kutunga nje ya Kizazi yaani ectopic pregnancy,
  • Kisonono kinaweza pia kusababisha shida ya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wa kujifungua(Njiti/premature)

(2) Ikiwa wewe ni Mwanaume,Kisonono kinaweza kusababisha:

  • kovu kwenye urethra
  •  Kupata jipu ndani ya uume wako, ambalo linaweza kuathiri uwezo wako wa kutungisha Mimba
  • Kupata tatizo la Epididymitis, au kuvimba kwa mirija ya kubebea shahawa karibu na korodani zako
  • Maambukizi ambayo hayajatibiwa yanaweza pia kuenea kwenye mfumo wako wa damu, ambapo yanaweza kusababisha matatizo adimu kutokea lakini makubwa kama vile ugonjwa wa baridi yabisi(arthritis) pamoja na uharibifu wa valve ndani ya moyo.

MATIBABU YA UGONJWA WA KISONONO

Ni vizuri kwenda hospital kufanyiwa vipimo kwanza kabla ya dawa, Na baada ya hapo kama utagundulika una tatizo hili basi utapata matibabu sahihi kulingana na ugonjwa wako pamoja na hatua ulipofikia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments