Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Utangulizi:

Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo chanzo chake ni utitiri mdogo sana yaani tiny burrowing mite ambao hujulikana kama Sarcoptes scabiei.  Mtu hupata muwasho sana kwenye eneo ambalo utitiri huo umechimba.

Na wakati mwingine hali huwa mbaya Zaidi nyakati za Usiku ambapo Utitiri huu huhitaji kuchimba Zaidi.

Scabies inaambukiza na inaweza kuenea haraka kupitia mawasiliano ya karibu ya mtu na mtu katika familia, kikundi cha watoto, darasa la shule, nyumba ya uuguzi au gereza n.k. Kwa sababu upele huenea kwa urahisi, wahudumu wa afya mara nyingi hupendekeza kutibu familia nzima au watu wowote wa karibu.”

SCABIES: Makala 

Scabies, ni ugonjwa wa ngozi unaohusishwa na kuwasha na madoa madogo mekundu kwenye ngozi, yanayosababishwa na utitiri wa kuwasha(itchy mite).

Aina ya Utitiri huu yaani tiny burrowing mite hujulikana kwa kitaalam kama Sarcoptes scabiei.

Dalili za Scabies

DALILI ZA UGONJWA WA SCABIES NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata muwasho sana kwenye ngozi yake, na sana sana muwasho huu huzidi sana wakati wa usiku

– Kuanza kupata upele kwenye ngozi

– Ngozi kuanza kuwa na madoa doa mekundu

– Na maeneo ya ngozi ambayo huweza kuathiriwa zaidi ni pamoja na;

• Kati kati ya vidole

• Eneo la kwapani

• Kuzunguka kiuno

• Kwenye mikono

• Chini ya miguu kwenye sole

• Kuzunguka maziwa au matiti

• Kwenye sehemu za siri za Mwanaume(Around the male genital area)

• Eneo la matakoni

• Kwenye magoti

• Na kwa upande wa watoto wadogo, sana sana hutokea kwenye kichwa(Scalp), viganja vya mikono pamoja na miguuni.

MATIBABU YA SCABIES

– Zipo njia mbali mbali za kutibu Ugonjwa huu wa Scabies pamoja na vitu vya kuzingatia na kufanya ukiwa nyumbani, ikiwemo swala la usafi wa mwili pamoja nguo zako,

Na kwa upande wa tiba huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo za kunywa au Cream za kupaka n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!