Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua

Mara nyingi watu wengi wakipata Shida ya kupumua kwa sababu ya pua kuziba hutumia Mdomo kupumua, Pua huweza kuziba kwa Sababu mbali mbali ikiwemo Mafua n.k

je, ni Sahihi Mtu kupumua kwa kupitia mdomo? Yapi ni madhara ya kufanya hivo? Soma hapa Makala hii Mpaka Mwisho kujua…

Fahamu tafiti mbali mbali zinaonyesha Kwa wastani mtu hupumua lita 10,000 hadi 12,000 za hewa kwa siku. Hewa hii pia inaweza kuwa na mchanganyiko wa vitu vingine mbali mbali ikiwemo; vumbi, bakteria, virusi na kuvu au Fangasi. Vyote hivi huweza kusafiri kwenye njia ya upumuaji na kufika hadi kwenye mapafu.

Bahati Nzuri ni kwamba, Mfumo wa Upumuaji huweza kusafisha uchafu wote huu na kukuweka katika hali ya Usalama Zaidi,

Kupitia mfumo wa upumuaji, ni chembe chembe ndogo tu chini ya mikroni tatu ambazo zinaweza kuingia kwenye mapafu.

Jinsi ambavyo Mfumo wa Upumuaji huchuja Uchafu Huu

Kwenye njia ya Upumuaji kuna Maelfu ya nywele nyembamba sana kuliko ncha ya Sindano,nywele hizi hufahamika kama Cilia. Kati ya 25 hadi 35 ya cilia hizi hupatikana kwenye kila seli ndani ya pua. Zina urefu wa mikroni tano hadi saba kila moja.

Zinapatikana kwenye seli, na huonekana kama brashi. Kazi yao ni kuzuia kupenya kwa viumbe vidogo ambavyo ni chini ya 0.5 mm kwa upana.

Matokeo yake, huchuja viini vidogo vidogo na kuvitoa kupitia pua.

Vichujio katika pua

Kwa upande mwingine, tishu kwenye pua pia hutumika kuchuja vijidudu vya hewa. Kamasi iliyopo pia inaruhusu baadhi ya viini kuingia mwilini. Kimsingi huruhusu vijidudu visivyo na madhara ndani ya mwili wetu.

KingaMwili

Pia fahamu kwamba Mfumo wetu wa kingamwili unaweza kupambana na kuzuia viini hatari vinavyovuka kupitia kamasi na kuingia mwilini.

Madhara ya Kupumua kwa Kutumia Mdomo badala ya Pua

Unachotakiwa kujua ni kwamba;Kazi kubwa ya Mdomo ni kula chakula,Hakuna nywele ndogo au cilia zinazoonekana mdomoni ili kuchuja hewa.

Na mfumo wa chakula hupambana na kuzuia vijidudu vinavyoingia kwa njia ya chakula ambavyo huweza kuathiri mwili wetu.

Ndiyo sababu hatupaswi kula chakula kupitia pua zetu. Hivyo basi, usivute hewa kupitia mdomo.

Hii ina maana pia ni rahisi wewe kuvuta na kuingiza ndani kwenye mwili wako vimelea vya magonjwa ambavyo huja kwa njia ya Hewa.

Nini hufanyika unapopumua kwa mdomo kwa muda mrefu?

Baadhi ya watu hupumua kupitia kinywa kutokana na mabadiliko fulani ya kijeni pamoja na matatizo ya njia ya hewa kwenye pua.

Kupumua kwa kinywa husababisha matatizo ya usingizi.

Hata hivyo, utafiti uligundua kuwa mifupa usoni mwa watoto ambao walipumua kwa muda mrefu kupitia midomo yao iliathirika.

Imedaiwa katika utafiti kwamba husababisha matatizo katika ukuwaji wa mifupa na meno.

Kwa watu wazima, hata hivyo, kupumua kwa kutumia kinywa kunaweza kusababisha maumivu ya misuli ya uso na shingo pamoja na maumivu ya kichwa.

Mwaka 2020 utafiti ulifanywa na Baraza Kuu la Vyuo vya Madaktari wa Meno na Stomatologists nchini Uhispania juu ya upumuaji wa kutumia mdomo.

Utafiti huo ulibaini kuwa nusu ya watoto wenye umri wa miaka 12 waliohusika walikuwa na matatizo ya meno.

Utafiti huo huo pia uligundua kuwa miongoni mwa watu wazima, shingo zinaweza kulazimika kuinama mbele kidogo ili kupumua, na kusababisha mshtuko wa misuli.

Ikiwa una shaka yoyote juu ya faida za kupumua kwa pua, jaribu kupumua kwa mdomo.

Ikiwa kupumua kwa pua ni suala la kawaida, kupumua kwa mdomo husababisha shinikizo au athari fulani mwilini.

Hata hivyo, wataalam wanapendekeza kwamba unaweza kupumua kwa mdomo tu katika hali ya dharura.

Editor:Afyaclass

Source:Bbc

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!