watu walio na afya bora ya utumbo wanaonekana kuwa na mifumo ya kinga inayostahimili magonjwa zaidi
Fahamu hapa Jinsi ya kuboresha Afya ya utumbo
Si rahisi kutambua utumbo wenye afya kutokana na muundo wake ukilinganisha na viungo vingine, na hakuna chombo kimoja ambacho kinaweza kutumika kupima afya ya utumbo.
Utumbo wetu umejaa vijidudu. Kulingana na wataalamu vijidudu hivyo vikiwekwa pamoja, vinaweza kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1.8.
Kuna bakteria bilioni 100 katika kila gramu ya yaliyomo kwenye matumbo.
Kwa nini ni muhimu kuwa na utumbo wenye afya?
Utumbo unaweza kuathiri “karibu kila kiungo mwilini”, anasema Dk Johnson.
Ubongo na utumbo vina mfumo Thabiti wa mawasiliano unaojulikana kama mhimili wa utumbo na ubongo.
Viungo hivi vinategemeana na kila Kimoja ni muhimu kwa kingine -
Utumbo wakati mwingine huitwa ubongo wa pili kwa sababu bakteria wanaweza kuathiri mienendo yetu kupitia Neurons milioni 100 kwenye utumbo.
Neurons ni seli zinazopatikana katika ubongo wetu na mfumo mkuu wa neva ambao huelekeza mwili wetu jinsi ya kuishi.
Utumbo wa nje unaweza hata kudhibiti hali yetu kwa kutoa vipitishio vya mawasiliano vinavyopatikana kwenye ubongo, kama vile serotonin.
Jukumu linalojulikana zaidi la utumbo ni kufyonza virutubisho kutoka kwa chakula.
"Hatuwezi kuwa tunapoteza maji na madini kwenye kinyesi," anaelezea Dk Venkatraman Krishna, daktari wa magonjwa ya tumbo nchini India.
Dk Megan Rossi, anayejulikana pia kama Daktari wa Afya wa Utumbo nchini Uingereza, anasema kukosekana kwa vijidudu vya utumbo sasa kumehusishwa na zaidi ya hali 70 tofauti za kiafya - kutoka magonjwa ya moyo, mishipa ya kupumua hadi magonjwa ya kinga ya mwili kama ugonjwa wa arheumatoid arthritis.
Takribani 70% ya seli zetu za kinga huishi kwenye sehemu ya utumbo, na "huwasiliana mara kwa mara" na mfumo wa kinga, anasema Dk Rossi.
Hii ndiyo sababu "watu walio na afya bora ya utumbo wanaonekana kuwa na mifumo ya kinga inayostahimili magonjwa zaidi", anaongeza.
Unawezaje kuimarisha afya ya utumbo?
Kufuatia utafiti uliofanywa na Mradi wa American Gut 2018, wataalamu walianza kuwashauri watu kula walau aina 30 ya lishe inayotokana na mimea kila wiki ili kukuza bakteria wanopatikana kwenye utumbo.
Hii sio tu ni pamoja na matunda na mboga, lakini pia vitu kama mbegu, viungo na karanga.
Dk Rossi anashauri watu kuongeza matunda katika lishe ili kuimarisha afya ya utumbo.
Lishe yenye nyuzinyuzi nyingi hutusaidia kujisikia kamili, husaidia usagaji chakula na kuzuia kuvimbiwa, kulingana na Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza, ambayo inapendekeza watu wazima kula gramu 30 ya nyuzi kwa siku.
Kuchagua mikate ya unga au punje badala ya nyeupe, na kuchagua wali wa kahawia au pasta ya ngano, kunaweza kuongeza ulaji wako wa nyuzi.
Chanzo kingine cha nyuzinyuzi ni pamoja na viazi ambavyoo havijamenywa (kama vile viazi vilivyookwa) na kunde kama maharagwe, dengu au mbaazi, ambazo zinaweza kuongezwa kwenye kitoweo, kari na saladi.
Vyakula vya prebiotic (aina fulani za nyuzi na wanga) vimepatikana ili kuhimiza ukuaji wa bakteria rafiki kwenye utumbo.
Baadhi ya vyakula hivyo ni ndizi, vitunguu, kabichi, nafaka, na zabibu.
Dk Hanisha Khemani, mtaalam wa magonjwa ya tumbo nchini Pakistan, anasema kuanzisha "mlo uliosawazishwa, na wenye virutubisho" katika miaka yetu ya 20 ni "muhimu kwa afya ya muda mrefu".
Ni vyakula gani Vibaya kwa utumbo
Matumizi ya vyakula vilivyochakatwa sana, pombe na tumbaku si mazuri kwa utumbo wako, aeleza Dk Krishna.
Chakula kilichochakatwa sana kina viambato ambavyo ama hukandamiza bakteria 'nzuri' au kuongeza bakteria 'mbaya'.
Kwa kuzingatia mahali ulipo ulimwenguni, huenda ukalazimika kuacha kununua vyakula kutoka kwa wachuuzi wa mitaani wasiozingatia usafi hasa wa kuosha matunda na mboga ili kujikinga dhidi ya virusi au bakteria hatari, Dk Krishna anaongeza.
Anasisitiza uchafua matumbo yetu, na inaweza kuongeza asidi na vidonda vya tumbo.
Dkt Johnson anasema watu walio na mfadhaiko zaidi huwa na vijidudu vidogo vya aina mbalimbali.
Maelezo|Source:Via Bbc
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!