Madhara Ya Soda Kwa Mama Mjamzito

 MADHARA YA SODA KWA MAMA MJAMZITO

Hili ni swali ambalo watu wengi wameniuliza, kwamba matumizi ya soda kwa mama mjamzito yana madhara yoyote au mama mjamzito anaruhusiwa kunywa soda? soma hapa chini kufahamu majibu yake

Matumizi ya soda mara moja moja kwa mama mjazito ambaye hana historia ya kupata shida yoyote wakati wa ujauzito hayana shida yoyote, ila matumizi ya Soda kila siku au mara nyingi zaidi yana madhara kwa mama mjamzito,

Lakini pia matumizi ya kiwango chochote cha soda pamoja na vinywaji vyote vyenye sukari sio salama kwa mama mjamzito ambaye ana shida ya kisukari cha mimba yaani Gestational Diabetes au yupo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari cha mimba.

Unywaji wa soda kila siku wakati wa ujauzito huweza kuongeza uwezekano wa mama mjamzito kupatwa na matatizo mbali mbali kama vile Kisukari cha Mimba yaani Gestational Diabetes,pamoja na kusababisha matatizo kwa mtoto pia kama vile shida ya mtoto kuzaliwa mkubwa zaidi yaani big baby,Asthma n.k

Kisukari cha Mimba yaani Gestational Diabetes huweza kusababisha mama mjamzito kupata shida wakati wa kujifungua,mtoto kuwa mkubwa zaidi kuliko kawaida pamoja na shida ya kushindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa mtoto baada ya kuzaliwa,

Pia Kisukari cha Mimba yaani Gestational Diabetes(GD) huweza kuongeza uwezekano wa Presha kuwa juu(high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na mama kuwa kwenye hatari ya kupatwa na kisukari type 2 baada ya kujifungua.

KUMBUKA; Pia unaweza kukatazwa matumizi ya soda kabsa wakati wa ujauzito kutegemea na aina za soda unazokunywa hapa nazungumzia soda zenye Caffeine yaani Caffeinated soda.

- Hii hutegemea na kiwango cha caffeine kilichopo kwenye soda mfano; kama umetumia soda zenye caffeine kuanzia miligram(mg) 35 mpaka 55, pia unashauriwa kuchunguza na kiwango cha caffeine kilichopo kwenye mlo unaopata kwa siku kama vile kwenye chai,Kahawa,Chocolate n.k Hii itakusaidia kuepusha kuzidisha kiwango cha Caffeine kwenye mwili wako,

Hali ambayo huweza kukuletea madhara zaidi hasa kipindi cha ujauzito wako.

Kwa Mujibu wa "AMERICAN COLLEGE OF OBSTETRICIANS AND GYNECOLOGISTS(ACOG)" wameshauri kwamba, kiwango cha Caffeine unachotakiwa kukipata wakati wa ujauzito kisizidi 200 milligram(mg) kwa siku nzima.

Kumbuka,unavyotumia Caffeine inapita kwenye Placenta na moja kwa moja kwenda kwenye maji ya uzazi au Amniotic fluid pamoja na kwenye mzunguko wa damu wa mtoto aliyetumboni.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!