MAFUA YENYE DAMU,CHANZO NA TIBA
Hali hii ya kutoa mafua ambao yamechanganyika na Damu huweza kumtokea mtu yoyote kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
- Maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji yaani respiratory infection au tatizo la Nasal congestion
- Hali ya kupenga makamasi kwa nguvu mara kwa mara huweza kusababisha mishipa midogo sana ya damu ndani ya pua kupasuka na kuanza kuvuja damu,
hali ambayo huweza kusababisha mtu mwenye mafua kutoa makamasi ambayo yamechanganyika na damu,
Lakini pia mtu ambaye hupiga chafya sana mara kwa mara au kukohoa sana huweza kutokewa na tatizo hili la mishipa midogo midogo ya damu ndani ya pua kupasuka na kuanza kuvuja damu,
hali ambayo huweza kusababisha mtu mwenye shida ya mafua kutoa makamasi ambayo yamechanganyika pamoja na damu
- Tatizo la nasal congestion au respiratory infection,allergic reaction,sinusitis n.k
- Shida ya kimaumbile ya puani yaani anatomical abnormality mfano; shida ya deviated septum(tundu kwenye septum),bony spurs au kutokea fracture ndani ya pua,
- Hali ya pua kukauka kuliko kawaida au kukosa unyevu unyevu unaotakiwa ndani ya pua(moisture)
- Kuumia au kufanyiwa upasuaji puani,hali hii huweza kusababisha damu kuvuja puani hasa wakati unapenga makamasi
- Mishipa midogo midogo puani huweza kupasuka kutokana na matumizi ya vitu kama Coccaine au kuwa exposured kwenye mazingira yenye chemicals kama vile Ammonia,
hali hii huweza kusababisha damu kuvuja ndani ya pua na kuchanganyika na makamasi kwa mtu mwenye mafua
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile Asprin au Warfarin ambazo huweza kuathiri uwezo wa damu kuganda,
hali hii huweza kusababisha damu kuvuja ndani ya pua na kuchanganyika na makamasi kwa mtu mwenye mafua
- Shida ya Tumor,uwepo wa vimbe ndani ya kuta za pua huweza kuchangia shida hii ya damu kuvuja japo kwa asilimia ndogo sana
MATIBABU YA SHIDA HII
Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake kama nilivyo kwisha kuelezea hapo juu, hivo kutana na wataalam wa afya kujua chanzo cha shida hii pamoja na kupata tiba sahihi kwako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!