MJAMZITO KUKOJOA MARA KWA MARA
Wanawake baada ya kupata ujauzito huweza kupatwa na hali ya kukojoa mara kwa mara, je hali hii hutokana na nini?
Kukojoa mara kwa mara kwa mwanamke mjamzito wakati mwingine inaweza ikawa ni kawaida kabisa kama hakuna maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI,
Kwanza kabisa kitu muhimu cha kufahamu ni kwamba Mfuko wa uzazi (uterus) upo karibu kabisa na mfuko wa mkojo (urinary bladder)
Kwa ukaribu huu wakati mtoto anakuwa kichwa chake au sehemu nyingine ya mwili hutegemea na mlalo wa mtoto huweza kukandamiza kibofu cha mkojo hivyo husababisha mama kuhisi mkojo mara kwa mara.
Kumbuka kuna magonjwa mengine yanaweza kusababisha kukojoa mara kwa mara kama sukari na U.T.I
kwahyo kwa mama mjamzito anayepitia hali hii ni vizuri ukafika katika kituo cha kutolea huduma kwa uchunguzi wa kitaalamu kabisa
KUMBUKA: Kukojoa mara kwa mara asilimia kubwa ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito kutokana na sababu hapo juu,
ila sio kila kukojoa mara kwa mara ni kawaida, kufanya vipimo na kujiridhisha ni vizuri zaidi kwako,
#afyaclass #uzazisalama #inawezekana
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!