MSTARI MWEUSI TUMBONI KWA MJAMZITO

 MSTARI MWEUSI TUMBONI KWA MJAMZITO

Baadhi ya wanawake wajawazito hushangaa mbona wana mstari mweusi tumboni,

na nimekuwa nikipata maswali mbali mbali mfano;

Je hili ni tatizo au kawaida?

Je chanzo chake ni nini? n.k

Wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi sana hutokea kwenye mwili wa Mwanamke, mabadiliko hayo huhusisha maeneo mbali mbali ya mwili ikiwa ni pamoja na NGOZI.

Kuna maeneo ya ngozi huanza kupata rangi nyeusi zaidi ambayo haikuwepo hapo mwanzo kama vile kuzunguka chuchu kwenye matiti,kuonekana kwa mstari mweusi tumboni n.k

MSTARI MWEUSI TUMBONI KWA MJAMZITO(CHANZO CHAKE)

NB:Watu wengi hawajui kwamba mstari huu upo siku zote ila unakuwa haujapata rangi sana ya kuufanya uonekane kwa nje,

Ukiwa kwenye rangi hyo ya kutokuonekana(nyeupe) hujulikana kwa kitaalam kama Linea alba, ila baada ya kuwa na rangi(brown,nyeusi) huonekana sana kwa nje,na hapo ndipo kwa kitaalam hujulikana kama Linea Nigra.

CHANZO CHAKE

Mstari huu hupata rangi nyeusi au brown na kuufanya uonekane kwa nje kutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo vya estrogen na progesterone, ambapo mwili wako huzalisha kwa wingi sana vichocheo hivi wakati wa ujauzito ili kumsaidia mtoto kwenye ukuaji wake tumboni.

Vichocheo hivi vya Estrogen na progesterone hustimulate Seli hai kwenye ngozi yako ambazo kwa kitaalam huitwa melanocytes,

Hali ambayo husababisha melanocytes kuzalisha zaidi au kwa wingi melanin, pigment hii ya Melanin ndyo hubadilisha rangi kwenye ngozi na kuifanya nyeusi zaidi.

Hivo kadri melanin inavyozalishwa kwa wingi zaidi ndivo maeneo mbali mbali ya ngozi yako kama vile kuzunguka chuchu,mstari tumboni n.k hupata rangi nyeusi zaidi ambayo haikuwepo hapo mwanzo.

Mabadiliko hayo kwenye ujauzito ndyo hufanya Mama mjamzito kuonekana ana MSTARI MWEUSI tumboni,hali ambayo ni kawaida na wala sio tatizo kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!