Tatizo la Kichomi,Chanzo,Dalili na Tiba Yake
Kichomi ni tatizo la maumivu ya Kifua(chest pain) ambayo huweza kuambatana na kushindwa kupumua,kuhisi kuungua,kifua kizito n.k kulingana na chanzo chake.
CHANZO CHA TATIZO LA KICHOMI
Tatizo la kichomi huweza kuhusisha shida ya mapafu,moyo n.k
1. Maumivu ya kifua(Kichomi) kutokana na shida kwenye moyo huweza kusababishwa na;
• Kuzuiwa kwa damu kwenda kwenye moyo,
tatizo la shambulio la Moyo(Heart attack)
• Kuzuiwa au kuziba kwa mishipa ya damu kwenda kwenye Moyo,
tatizo la Chembe ya Moyo(angina)
• Kuvimba kwa moyo yaani pericarditis,myocarditis n.k
• Magonjwa kwenye misuli ya moyo kama vile cardiomyopathy
• Matatizo kwenye mshipa wa Aorta kama vile; aortic dissection n.k
Vyote hivi huweza kupelekea Tatizo la kichomi.
2. Tatizo la Kichomi kutokana na shida kwenye mfumo wa Umeng'enyaji chakula kama vile;
- Shida ya Gallstones
- Tatizo la Acid Reflux, kiungulia
- Matatizo ya kushindwa kumeza vitu kutokana na shida kwenye esophageal
- Kuvimba kwa kongosho(Pancrease), Gallbladder n.k
3. Tatizo la Kichomi(Maumivu ya Kifua) kutokana na matatizo ya Mapafu kama vile;
- Shida ya bronchospasms ambayo hutokea sana kwa Wagonjwa wa Asthma na matatizo mengine kwenye mapafu kama vile;chronic obstructive pulmonary disease (COPD)
- Tatizo la pneumonia, pneumothorax
- Shida ya viral bronchitis
- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama bacteria,virusi n.k kwenye vifuko vya hewa(Alveoli), mapafu n.k
- Shida ya damu kuganda,damu kutengeneza Clots na kusababisha tatizo la pulmonary embolism n.k
4. Tatizo la Kichomi kutokana na tatizo kwenye mbavu au matatizo ya kuvunjika(Rib- or fracture-related chest pain) kama vile;
- Mtu Kuvunjika mbavu
- Mbavu kuwa na vidonda
- Mtu kubanwa sana Mbavu n.k
5. Tatizo la Kichomi kutokana na tatizo la Wasiwasi(Anxiety-related chest pain)
Hii huweza kuhusisha maumivu ya kifua(kichomi), mapigo ya moyo kwenda mbio,kukosa pumzi,kutoa sana jasho,kupumua kwa haraka sana n.k
DALILI ZA TATIZO HILI LA KICHOMI
Dalili za Tatizo la kichomi zinaweza kugawanywa kulingana na chanzo chake kama nilivyoeleza hapo juu,ila kwa Ujumla ni kama vile;
- Mtu kupata maumivu makali ya Kifua
- Mtu kushindwa kupumua
- Mtu kuhisi Kifua kuwa Kizito Sana
- Mtu kuhisi hali ya kuungua Kifuani
- Mtu kutoa jasho Sana
- Mtu kupata kizunguzungu
- Mtu kuhisi kichefuchefu na Kutapika
- Mtu kupata maumivu ya kifua wakati wa Kumeza kitu n.k
VIPIMO Kwa Mtu mwenye Tatizo la kichomi
Unaweza kufanya baadhi ya Vipimo kama una Tatizo la kichomi, Vipimo hivo ni ikiwemo;
• Electrocardiogram or ECG
• Blood tests
• Chest X-ray
• Echocardiogram
• Computerized tomography or CT scan n.k
MATIBABU ya Tatizo la kichomi
Tiba ya Tatizo la kichomi hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla huweza kuhusisha;
- Matumizi ya Dawa mbali mbali kama vile;
Artery relaxers: Nitroglycerin, Propranolol, Asprin n.k
- Huduma ya Upasuaji n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!