TATIZO LA MAJI YA UZAZI KUPUNGUA,CHANZO NA TIBA

 TATIZO LA MAJI YA UZAZI KUPUNGUA,CHANZO NA TIBA

Tatizo hili huhusisha kupungua kwa maji ya uzazi maarufu kama Amniotic fluid na tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama OLIGOHYDRAMNIOS,

wakati wa ujauzito,maji haya ya uzazi au amniotic fluid hufanya kazi mbali mbali kama vile; kumlinda mtoto na aina yoyote ya msuguano au injury,na kutengeneza eneo la kutosha kwa ajili ya ukuaji wa mtoto pamoja na maendeleo yake,

Maji haya ya uzazi pia husaidia umbilical cord kutokugandamizwa,hii ni muhimu sana ili kuwezesha usafirishaji mzuri wa nutrients,hewa safi ya oxygen pamoja na damu kwenda kwa mtoto

KUMBUKA; kiwango cha maji ya uzazi(amniotic fluid) kilichopo hutegemea na kiwango cha maji ya uzazi kinachozalishwa pamoja na kiwango cha maji ya uzazi kinachotolewa kutoka kwenye amniotic sac.

KWENYE MIEZI MITATU YA MWANZO(first trimester)- Chanzo kikubwa cha maji ya uzazi ni kutoka kwenye mapafu ya mtoto yaani fetal lung secretions pamoja na usafirishaji wa Plasma kutoka kwa mama ambao hupitia kwenye kondo la nyuma yaani placenta pamoja na fetal membrane

KWENYE MIEZI MITATU YA PILI(second trimester)- Figo za mtoto yaani fetal kidneys huanza kuzalisha mkojo ambao huwa chanzo kikubwa cha maji ya uzazi kwa kipindi hicho pamoja na kipindi chote killichobakia cha ujauzito

VIPIMO
Tatizo hili la kupungua kwa maji ya uzazi kipindi cha ujauzito yaani OLIGOHYDRAMNIOS hugungulika kwa kupitia vipimo kama vile ULTRASOUND.

CHANZO CHA MAJI YA UZAZI KUPUNGUA

1. Sababu kwa Upande wa Mama mwenyewe

- Mama kuwa na matatizo mbali mbali ya kiafya kipindi cha ujauzito kama vile;

• Tatizo la kifafa cha mimba yaani preeclampsia and eclampsia

• Kuwa na tatizo la presha ya muda mrefu yaani Chronic hypertension

• Uwepo wa magonjwa kama vile Collagen vascular diseases,nephropathy thrombophilia n.k

Matatizo kama haya huweza kupunguza mzunguko wa damu yaani Blood flow kwenda kwenye viungo muhimu mbali mbali vya mtoto aliyetumboni kama vile placenta,

hali ambayo huweza kupelekea kuathiri kwa uzalishwaji wa mkojo kwa mtoto,na kusababisha tatizo la kupungua kwa maji ya uzazi yaani OLIGOHYDRAMNIOS

• Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile Angiotensin converting enzyme inhibitors(Lisinopril),prostaglandin synthetase inhibitors(NSAIDs) n.k huweza kupunguza flow ya damu kwenda kwenye kibofu cha mkojo kwa mtoto kisha kuathiri uzalishwaji wa kutosha wa mkojo na kupelekea tatizo la kupungua kwa maji ya uzazi au OLIGOHYDRAMNIOS

• Mama kutokunywa maji ya kutosha kipindi cha ujauzito hasa kwenye vipindi vya hali joto au summer seasons

• Maambukizi ya magojwa mbali mbali kama vile magonjwa ambayo yapo kwenye kundi la TORCH ikiwa na maana ya; toxoplasma,gondii,Rubella,cytomegalovirus,herpes simplex virus,parvovirus B19.

2. Sababu kwa upande wa mtoto mwenyewe

- Matatizo kwenye vinasaba yaani chromosomal abnormalities kama vile Down syndrome

- Matatizo kwa mtoto kama vile shida ya Renal agnesis,cystic renal disease n.k ambayo huhusiana na kuathiri uzalishwaji wa mkojo,kisha kusababisha tatizo la kupungua kwa maji ya uzazi yaani OLIGOHYDRAMNIOS

- Mtoto kukaa tumboni kwa muda mrefu kuliko mda ulitorajiwa kuzaliwa yaani post-term pregnancy

- Shida ya kupasuka kwa chupa ya uzazi yaani rupture of membranes

- Shida ya mtoto kutokukuwa akiwa ndani ya tumbo la uzazi yaani intrauterine growth restriction(IUGR)

- Tatizo la Amnion nodosum, ikiwa na maana ya tatizo la kushindwa kuzalishwa kwa seli hai za amnion ambazo hufunika upande wa kondo la nyuma yaani placenta

3. Sababu za kwenye kondo la nyuma au placenta

- Tatizo la kondo la nyuma kuachia lilipojishikiza hali ambayo hujulikana kama placenta abruption

- Hali ambayo huhusisha uwepo wa mapacha yaani twin-twin transfussion

- Tatizo la placental thrombosis

- Tatizo la placental kushindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!