Ugonjwa wa fangasi ya ngozi,chanzo,dalili na Tiba yake
Maambukizi ya Fangasi kwenye ngozi kwa Lugha nyingine hujulikana kama mycosis
Kuna mamilioni ya aina za fungi ambao Wanaishi kwenye uchafu, kwenye mimea, kwenye nyumba,na kwenye ngozi yako. Wakati mwingine, fangasi hawa wanaweza kusababisha matatizo ya ngozi kama vile vipele au Rashes
Dalili za Fangasi kwenye Ngozi
Baada ya kushambuliwa na Fangasi kwenye Ngozi,Zipo dalili mbali mbali ambazo huweza kujitokeza kwako, dalili hizo ni pamoja na;
- Kupata muwasho kwenye ngozi
- Ngozi kutoka magamba(Scaly skin)
- Ngozi kuwa nyekundu eneo lililoathiriwa
- Ngozi kuwa na Vipele au rashes
- Kuvimba
- Ngozi kuwa na vitu kama mashilingi(Tazama kwenye picha)
- Kupata dalili ya malengelenge kwenye ngozi
- Ngozi kutoa Unga n.k
Aina ya Fangasi kwenye Ngozi
Zipo aina mbali mbali za Fangasi kwenye ngozi,na baadhi ya aina hizo ni pamoja na;
1.Athlete’s foot au tinea pedis:
Hii ni aina ya Fangasi ambao hushambulia Miguu.Fangasi hustawi katika mazingira yenye joto na unyevunyevu kama vile kwenye viatu, soksi, mabwawa ya kuogelea, vyumba vya kubadilishia nguo, na sehemu ambapo wanaoga watu wengi.
Maambukizi haya ni ya kawaida zaidi kwa watu wanaovaa viatu vinavyobana miguu, watu ambao hawabadili soksi mara kwa mara, na kutumia bafu za umma au mabwawa. Kuvu au Fangasi wanaohusika wanaweza huishi kwenye tishu zilizokufa za nywele, kucha za miguu, na tabaka za nje za ngozi, huku Trichophyton rubrum wakiathiri Zaidi maeneo haya.
2. Jock itch au tinea cruris:
Hii ni Aina ya fangasi inayoitwa tinea ambayo husababisha maambukizi haya. Kuvu au Fangasi hawa hustawi katika maeneo yenye joto na unyevunyevu kama vile sehemu za siri, mapajani na matakoni.
Maambukizi ni ya kawaida zaidi wakati wa majira ya joto au katika hali ya hewa ya joto na ya mvua. Jock itch inaonekana kwa dalili kama vile;
- Kupata upele mwekundu kwenye ngozi,
- kupata muwasho wa ngozi,
- kuwa na upele wenye umbo la pete kwenye ngozi(ring-shaped rashes)n.k.
Jock itch inaambukiza kwa kiasi kidogo tu, inaenea kwa mgusano wa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia vitu vilivyobeba kuvu au fangasi hawa. Dalili ni pamoja na:
✓ Kupata muwasho au hali ya kuwaka moto katika eneo la sehemu za Siri au kwenye mapaja
✓ Upele mwekundu wa mviringo na kingo zilizoinuliwa,
✓ Hali ya uwekundu,Kuchubuka, au kupasuka kwa ngozi n.k
3. Ringworm, or tinea corporis:
Ringworm, au tinea corporis, ni maambukizi ya Fangasi wa ngozi yaliyopewa jina kutokana na upele wake wenye umbo la pete na ukingo unaofanana na minyoo.
Fangasi hawa huambukiza na wanaweza kuenea kwa kugusana moja kwa moja na watu walioambukizwa au wanyama au kwa kugusa nguo au samani zilizochafuliwa.
Joto na unyevu vinaweza kusaidia kuenea kwa maambukizi. Dalili zake ni pamoja na;
- kidonda chekundu, cha duara na bapa chenye ngozi ya magamba – ambapo sehemu ya nje ya kidonda inaweza kuinuliwa, huku katikati ikionekana kawaida.
- Upele mithili ya Pete nyekundu au viraka vinavyoweza kuingiliana.
3. Yeast infections:
Maambukizi ya fangasi hawa kwenye ngozi yako huitwa cutaneous candidiasis. Aina ya fangasi iitwayo candida husababisha maambukizo haya inapokua sana.
Mara nyingi fangasi hawa hupatikana katika sehemu zenye joto, unyevunyevu, zilizopasuka za mwili wako, ikijumuisha kwapani,sehemu za siri au kwenye kinena. Mara nyingi hutokea kwa watu wenye fetma au ugonjwa wa kisukari. Pia, ikiwa unatumia antibiotic, kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya chachu yaani yeast infection.
4. Onychomycosis:
Onychomycosis ni maambukizi ya Fangasi ambayo huathiri sana kwenye vidole vya miguu au vidole vya mikono. Maambukizi haya Husababisha kucha zako kubadilika rangi, kuwa nene, na wakati mwingine kujitenga na eneo la kucha kujishikiza.
Hali hiyo ni ya kawaida zaidi kwa watu wazima kutokana na matatizo kama vile mtiririko mbaya wa damu, matatizo ya mfumo wa kinga, na kisukari. Onychomycosis huathiri kucha za Miguu mara nyingi zaidi kuliko kucha za Vidole kwa sababu hukua polepole zaidi, huwa na mtiririko mdogo wa damu, na kwa kawaida huwa katika hali ya giza na unyevu unyevu.
Uvaaji wa Viatu vinavyobana sana,Soksi chafu au zenye unyevu unyevu,hukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi haya.
Sababu zinazoongeza Hatari ya kupata Maambukizi ya Fangasi kwenye Ngozi;
Una uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya Fangasi kwenye ngozi ikiwa:
– Unamawasiliano ya karibu au kugusana(Close contact) na mtu au mnyama aliyeambukizwa
– Unaazima viatu au nguo ambazo zina fangasi hatari
– Unatumia dawa jamii ya antibiotics kwa muda mrefu Zaidi
– Una uzito kupita kiasi
– Una magonjwa kama kisukari
– Unatatizo la kutoa jasho sana
– Unavaa Viatu vinavyobana sana,Soksi chafu au zenye unyevu unyevu
– Kuwa na mfumo wa kinga dhaifu
– Kuishi katika mazingira ya joto au mvua
– Unavaa nguo za kubana au viatu ambavyo havina mzunguko mzuri wa hewa n.k.
Matibabu ya Fangasi hawa
Zipo Dawa za antifungal za aina mbali mbali za kupata yaani Topical antifungals, na Za Vidonge vya Kunywa,
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!