UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI-MUMPS)
UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI-MUMPS)
Ugonjwa wa kuvimba mashavu maarufu kama Matumbwitumbwi,ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Mumps,
ugonjwa huu huhusisha kuvimba kwa tezi la Mate yaani Salivary gland ambalo lipo karibu na sikio lako,
Ugonjwa wa kuvimba mashavu huweza kuhusisha mtu kuvimba shavu la upande mmoja au kuvimba mashavu yote mawili
CHANZO CHA UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU
Ugonjwa wa kuvimba mashavu au matumbwitumbwi, ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Mumps,hutokana na maambukizi ya Virusi yaani Viral infection ambayo hushambulia kwanza sehemu ya tezi la mate yaani Salivyary gland, ndipo baadae huweza kusambaa katika maeneo mengine.
Mtu huweza kupata virus hawa wa Mumps kutoka kwa mate ya mtu mwenye virusi akiwa anakohoa,kupiga chafya au kwa njia yoyote ile ambayo huweza kuhusisha mate kugusana.
DALILI ZA UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU
- Baadhi ya watu hawaonyeshi dalili zozote baada ya kuambukizwa na Virusi wa mumps, Lakini wengi wao huonyesha dalili ambazo huanza kuanzia wiki 2 mpaka 3 baada ya kupatwa na virusi hawa wa Mumps.
• Dalili ya kwanza kabsa ni mtu kuvimba shavu moja au mashavu yote mawili kutokana na kuvimba kwa tezi la mate(salivary gland)
• Mtu kupata maumivu ya shavu lililovimba
• Mtu kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu chochote au kupiga miayo
• Joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na homa
• Mtu kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara
• Mtu kupata maumivu ya misuli,joints na viungo mbali mbali vya mwili
• Mwili kuchoka kupita kiasi
• Mtu kukosa kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote n.k
MADHARA YA UGONJWA HUU WA KUVIMBA MASHAVU AU MUMPS NI PAMOJA NA:
- Mtu kuvimba korodani moja au zote mbili hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Orchitis
- Mtu kuvimba ubongo,hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Encephalitis
- Kuvimba kwa ngozi pamoja na uwepo wa maji zaidi kwenye ubongo pamoja na uti wa mgongo,maambukizi ambayo hujulikana kama meningitis
- Mtu kuvimba kongosho,hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama pancreatitis
- Mtu kupoteza uwezo wake wa kusikia kwa sikio moja au yote mawili
- Mtu kupatwa na matatizo mengine ya moyo
- Mwanamke kupatwa na tatizo la mimba kutoka zenyewe hasa kwenye miezi mitatu ya mwanzoni n.k
JINSI YA KUZUIA UGONJWA HUU WA KUVIMBA KWA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI AU MUMPS)
✓ Ugonjwa huu huzuiwa kwa njia ya chanjo, ambapo kwa kawaida chanjo yake hutolewa kwenye mfumo wa combined yaani, Measles-mumps-Rubella(MMR),
Dose zake hutolewa mbili yaani;
-Mtoto akiwa na mri wa kati ya miezi 12 na 15
- Pamoja na mtoto akiwa na umri wa kati ya miaka 4 na 6
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!