UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE(paronychia)

 UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE(paronychia)

Ugonjwa wa paronychia ni ugonjwa ambao kwa huku kwetu ni maarufu kwa jina la ugonjwa wa mdudu kwenye kidole, ugonjwa huu huhusisha maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa(WADUDU) kama vile Bacteria au Fangasi kwenye ngozi ndani ya kidole hasa karibu na eneo la kucha yako.

Tafiti zinaonyesha ugonjwa huu huwapata sana watu wanaofanya kazi kwenye mazingira ya kushika maji sana mara kwa mara au watu ambao ni rahisi kuwa katika mazingira yenye kemikali za vitu mbali mbali kama madawa ya shambani,viwandani n.k  na watu hao ni kama vile;

1) Wanawake wafanyakazi Wa ndani yaani housegirl
2) wanaume wafanyakazi Wa ndani yaani houseboy
3) wajenzi
4) wakulima
5) wanaofanya mapenzi kwa kutumia vidole mara kwa mara

Makundi mengine ni kama vile; Wanawake wanaofua nguo Mara kwa Mara,wanaopenda kung'ata kucha,wenye upungufu Wa kinga mwilini ikiwemo wagonjwa wa kisukari,UKIMWI,saratani au kansa n.k

DALILI ZA UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE

Tatizo hili la mdudu kwenye kidole au Paronychia huweza kuhusisha dalili mbali mbali kama vile:

- Mtu kupata maumivu pamoja na kuvimba kidole

- Kidole kubadilika rangi na kuwa na wekundu kuzunguka kucha

- Eneo karibu na kucha kujaa usaha

- Kucha kuwa ngumu kuliko kawaida

- Kucha kuanza kutoka(kwa baadhi ya watu)

- Kucha kuanza kujitenga kutoka kwenye sehemu yake yaani nailbed n.k

CHANZO CHA UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE

Ugonjwa huu wa mdudu kwenye kidole au paronychia husababishwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa au WADUDU kama vile Bacteria na Fangasi kwenye ngozi kuzunguka kucha ndani ya kidole, Bacteria ambao wanaongoza kusababisha tatizo hili hujulikana kama Staphylococcus aureus na Streptococcus pyogenes bacteria

Lakini pia tabia kama vile; Mtu kung'ata kucha mara kwa mara huongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili, hii ni kwa sababu kung'ata kucha huweza kusababisha ngozi ya kwenye kucha au karibu sana na kucha kutengeneza uwazi,mchubuko au vitundu ambavyo itakuwa rahisi sana kwa vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria au fangasi kupenya kwa urahisi zaidi,Tatizo hili huweza kumpata mtu wa umri wowote na linatibika kabsa.

MATIBABU YA UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE

Matibabu ya tatizo hili hutegemea na ukubwa wa tatizo, je ni la muda mrefu au muda mfupi n.k,

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!