Ugonjwa wa Mpox,Chanzo,Dalili na Tiba
Ugonjwa wa Mpox,Chanzo,Dalili na Tiba
Ugonjwa huu kwa jina Lingine hujulikana kama Homa ya nyani, Mpox hapo awali ilikuwa inajulikana kama MonkeyPox, Hawa ni Virusi ndyo wanaosababisha Ugonjwa huu
Jinsi Ugonjwa wa Mpox,Homa ya Nyani husambaa
Ugonjwa wa Mpox unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo;
- kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa
- na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi
- ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu.
- Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Dalili za Ugonjwa wa Mpox,Homa ya nyani
Dalili kuu ya Mpox ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.
Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa Mpox
Ugonjwa huu haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa kutekeleza yafuatayo;-
i. Kutoa taarifa kupitia namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Mpox.
ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.
iii. Kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana mtu mwenye dalili za Mpox.
iv. Kuepuka kugusana na mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.
v. Kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.
vi. Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.
vii. Safisha na kutakasa vyombo vilivyotumika na mhisiwa au mgonjwa pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara.
viii. Kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Mpox.
ix. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Mpox.
x. Watoa huduma za afya kuzingatia miongozo ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi (IPC) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.
Via:WizaraafyaTz
2 Comments
Asante sana kwa Elimu hii Mtaalam
ReplyDeleteSawa sawa
DeleteWEKA COMMENT HAPA..!!!