Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa visunzua,chanzo,dalili na Tiba yake



 Ugonjwa wa visunzua,chanzo,dalili na Tiba yake

VISUNZUA ni vinyama vinavyoota kwenye ngozi ambavyo husababishwa mara nyingi na maambukizi,matatizo ya homoni wakati wa ujauzito au unene kupita kiasi.

Visunzua kwa wengine huita "Warts" ambazo husababishwa na maambukizi ya Virusi vya Human Papilloma Virus(HPV)(Tazama kwenye picha hapa)

•Soma zaidi hapa juu ya Warts:Link to Source

Matatizo ya ngozi hutofautiana sana kuanzia kwa dalili na athari ikiwemo ukali. Baadhi huwa ya muda au ya kudumu ilhali mengine hutoweka baada ya muda mchache.

Visunzua ni vinyama vinavyoota juu ya ngozi ambapo vinaweza kutokea maeneo kama vile;

  • usoni,
  • kuzunguka jicho,
  • shingoni,
  • mgongoni na kadhalika.

Vinayama hivyo ambavyo baadhi huviita
visunzua vinakuwa kama alama na vijinyama hivyo vinapoota kwenye ngozi
huwa laini na hutofautiana kwa rangi:
Kawaida huwa na rangi inayofanana na
ngozi ya mtu, vinaweza kuwa rangi ya
kahawia lakini mara nyingi hufuata rangi
ya mtu aliyonayo.

Baadhi ya vinyama hivyo wakati
mwingine hubadilika rangi na kuwa
vyekundu au vyeusi kama mtu aliyenavyo
ataamua kuviminya minya.

wakati mwingine Vinyama au alama hizo aghalabu huwezi kuviona kwa urahisi bila kutumia kifaa maalumu (Microscopic),
vingine hukua mpaka kufikia urefu wa milimita tano au zaidi.

Lakini watu wengine huvigundua kwa sababu huwa vinawasha vinapogusana na nguo.

Visunzua au vinyama vyeusi husababishwa na matatizo ya homoni wakati wa ujauzito au unene kupita kiasi.

Matibabu yake hufanyika hospitalini ambapo vinatolewa na vifaa maalumu.

Pia unaweza kuvitibu nyumbani kwa njia za asili.

Mtu anaweza kuota kinyama kimoja au zaidi sehemu moja, iwapo mahali kinapoota itakuwa imejificha au
imejikunja kama vile chini ya matiti, pembeni au mgongoni ambako sio rahisi kuviona au asijue kama ameota vinyama hivyo mpaka awe mara kwa mara anapooga anajisugua sehemu zote za mwili au kwa kujiangalia kwenye kioo kwa makini.

"Vinyama kwenye ngozi havina madhara, hata hivyo vinaweza kusababisha maumivu kutokana na muwasho na msuguano unaotakana na nguo au vito
ma hereni, bangili au mkufu," anafafanua Daktari Nkanyezi Ferguson, ambaye ni Profesa na mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kutoka Chuo Kikuu cha Uuguzi,
lowa.

Vinyama hivi huota karibu nusu ya watu wenye umri mkubwa, hupendelea kuota zaidi kwa watu wanaoelekea kuwa wazee,

Watu wanene sana wako kwenye nafasi kubwa ya kupata vinyama hivyo kwa sababu ya kuwa na ngozi iliyojikunja kunja.

Vinyama hivi huota kwa kurithi. Kama kwenye familia yako kuna mtu mwenye vinyama hivyo, mwingine
anaweza kuvipata. "Wanaume na wanawake huathirika
sawa sawa," anasema Dk. Ferguson.

Lakini kuna sababu nyingine ukiwa mnene sana kupata vinyama hivi, kwa sababu unakuwa kwenye hatari ya
kupata ugonjwa wa kisukari (type 2 diabetes) na utafiti umegundua kuwa mtu mwenye aina hiyo ya kisukari
anapata vinyama vingi, kama ilivyo kwa watu wenye sukari ya juu sana.

Kutokana na hali hiyo kuna uhusiano kati ya vinyama kwenye ngozi na insulini ambayo inadhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.

"Insulini inachochea ukuaji na kusababisha seli ya ngozi kubadilika. Hali hii kufanya vinyama kuendelea kuongezeka ambayo ni dalili ya kisukari," anaongeza Dk. Courgi.

"Watu wanene sana wenye kisukari wako kwenye uwezekano wa kuota vinyama kwa sababu ya kiwango kikubwa cha insulini,” anaeleza Daktari Robert Courgi,
kutoka Hospitali ya Long Island, NewYork.

Vinyama hivi vinaweza kuondoka vyenyewe. Lakini kwa kawaida, mara vinapojitokeza, huwa na kawaida ya
kubaki kwenye ngozi.

"Hakuna sababu za kitabibu zinazolazimisha kuondoa vinyama, ni sawa tu kama utaviacha," anasema Dk.
Ferguson. "Unaweza kuviondoa kama vitakuwa vinasumbua.”

Mtu inambidi amuone mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kuhakikisha anaondolewa kwa njia salama na
daktari.

Unapotaka kuviondoa vinyama kumbuka kuwa vimegusa mwili, lazima uwe muangalifu, usifikiri kuwa unaweza kuvikata kwa mkasi kirahisi, vinaweza
kusababisha maumivu, kuvuja damu na uwezekano wa kupata maambukizi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments