Ukimeza Big G,inakaa tumboni kwa Miaka 7, Madhara yake ni nini?
Baadhi ya Watu wamekuwa wakiamini kwamba,kama ukimeza Big G basi inauwezo wa kukaa tumboni kwako kwa kipindi cha Miaka 7, Je ni kweli?
Ukweli ni kwamba hushauriwi Kumeza Big G baada ya kuona utamu umeisha au umemaliza kuitumia,
Lakini je nini kinaweza kutokea pale ambapo umemeza kipande kidogo cha Big G, Maana watu wanasema Big G huwa haimeng'enywi kabsa tumboni.
SOMA HAPA;
kwanza Big G(Gum) inaweza kutoka kwenye miti yaani tree resin au kutengenezwa na gum base, ambapo kwa asilimia kubwa vitu hivi havifanyiwi umeng'enyaji tumboni kama ilivyo kwa vyakula vya kawaida unavyokula.
Sasa basi kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Mwili, Kama vitu hivi havifanyiwi umeng'enyaji basi husubiri wakati wa Kutolewa Nje kwa Njia ya Haja Kubwa,
Baadhi ya Tafiti zinaonyesha"Endapo umemeza kipande cha Big G(Gum) kitatoka ndani ya Masaa 40 kupitia Njia ya Haja Kubwa, na kwa vile hakimeng'enywi basi kitatoka kama kilivyo" Anasema Mtaalam Mmoja anayejulikana kama Czerwony.
Hivo basi unashauriwa kutokumeza vitu kama hivi, japo vinaweza visikusababishie madhara yoyote Mwilini,
Kumeza kipande Kimoja cha Big G kwa bahati mbaya sio tatizo Ila endapo unameza vipande vingi mara kwa mara ndani ya kipindi kifupi cha Muda,huweza kuleta athari kwenye mfumo wako wa Umeng'enyaji chakula.
Kama unafanya hivi kila siku na mara nyingi zaidi ndani ya siku Moja,inaweza kusababisha tatizo la kuziba kwa Utumbo yaani intestinal blockage,
NENDA HOSPITAL HARAKA KAMA UMEMEZA BIG G(GUM) HALAFU UNAPATA DALILI HIZI HAPA;
1. Unapata Maumivu makali ya Tumbo
2. Kuanza kupata tatizo la choo kigumu pamoja na kujisaidia kwa shida sana(Constipation)
3. Kujihisi Umeshiba Muda wote
4. Tumbo lako kujaa au Kuvimba
5. Kuanza kupata shida ya Kutapika n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!