Afariki kwa Kutolewa ini Kimakosa Badala ya bandama

Afariki kwa Kutolewa ini Kimakosa Badala ya bandama

Mzee wa miaka 70 nchini Marekani, aliyefahamika kwa jina la William Bryan, amefariki akiwa kwenye chumba cha upasuaji, baada ya madaktari kumtoa kiungo kisicho sahihi wakati wa upasuaji.

Baada ya uchunguzi wa vipimo uliofanywa, na madaktari katika Hospitali ya Ascension Sacred Heart Emerald Coast walimshawishi mwanaume huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo, hata hivyo, mambo yalikwenda tofauti baada ya daktari kung’oa ini kimakosa wakati wa upasuaji wa kumtoa kiungo kingine chenye changamoto ambayo ni Bandama

Hata hivyo mambo yamekuwa magumu katika kesi iliyofunguliwa dhidi ya hospitali hiyo baada ya jopo la mawakili kudai kwamba Daktari Mkuu wa Upasuaji Dk Thomas Shaknovsky na Afisa Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt Christopher Bacani, waliishawishi familia iliyositasita mzee huyo wa miaka 70 kufanyiwa upasuaji hospitalini hapo na kwamba angeweza kupata matatizo makubwa ikiwa ataondoka hospitalini.

William Bryan na mkewe Beverly walikuwa wakitembelea nyumba yao ya kukodisha huko Florida mwezi uliopita mara ghafla alianza kupata maumivu ya tumbo la chini, kushoto na mara moja walienda katika Hospitali ya Ascension Sacred Heart Emerald Coast, ambapo mzee huyo wa miaka 70 alilazwa kwa uchunguzi zaidi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!