Bacteria wa Escherichia coli maarufu kwa kifupi cha E. coli,

Bacteria wa Escherichia coli maarufu kwa kifupi cha E. coli,

Hawa ni bacteria ambao hupatikana kwenye mazingira yetu,kwenye chakula,na ndani ya utumbo wa binadamu pamoja na wanyama pia.

Asilimia kubwa ya bacteria hawa wa E.coli hawana madhara kwa binadamu,badala yake uwepo wake ni muhimu kwa utumbo wa binadamu,

Japo,wapo baadhi yao huweza kusababisha matatizo kama vile kuharisha,Maambukizi kwenye njia ya mkojo(urinary tract infections-UTI), matatizo kwenye njia ya hewa yaani respiratory illness, maambukizo kwenye damu pamoja na madhara mengine.

Aina hii ya Bacteria wa E.coli ambao wanadhara huweza kusambazwa kupitia maji machafu, chakula, au kupitia kugusana na wanyama au binadamu.

Bacteria wa E.coli huwa na madhara pale ambapo huweza kuzalisha Sumu ambayo hujulikana kama Shiga toxin, na aina hii ya bacteria wa E.coli hujulikana kama Shiga toxin-producing E. coli

MADHARA YA BACTERIA HAWA WABAYA;

Hizi hapa chini ni baadhi ya Dalili ambazo huweza kujitokeza,endapo umeshambuliwa na bacteria hawa

1. Mtu kupata maumivu ya tumbo,tumbo kukaza sana(stomach cramps) n.k

2. Mtu kuanza kuharisha

3. Mtu kupata hali ya kichefuchefu na kutapika

4. Baadhi ya watu hupata HOMA

5. mwili kuchoka Sana Muda wote N.k

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA MADHARA KUTOKANA NA AINA HII YA BACTERIA NI PAMOJA NA;

- Wakina Mama Wajawazito

- Watoto wachanga, na watoto wenye umri wa chini ya miaka 10

- Wazee

- Watu ambao hawana utaratibu wa kunawa Mikono mara kwa mara

- Pamoja na Watu wenye magonjwa ambayo hudhoofisha kinga ya Mwili kama vile; Ugonjwa wa Saratani,Kisukari, UKIMWI n.k

ZINGATIA MAMBO HAYO ILI KUJIKINGA NA BACTERIA HAWA WABAYA

• Hakikisha Mikono yako inakuwa Safi,Nawa mikono yako kwa maji Safi,tiririka pamoja na Sabuni, hasa baada ya kutoka chooni, kumbadilisha mtoto Nepi au kushika vitu mbali mbali

• Nawa mikono kabla na baada ya kula Chakula

• Nawa Mikono baada ya kutoka Safarini, n.k

• Pia jenga Utaratibu wa kutumia Sanitizer mara kwa mara kusafisha mikono yako.

KUMBUKA; Kinga kubwa ya tatizo hili ni USAFI,Nawa Mikono kwa maji Safi na Sabuni, na hakikisha kila kitu kinakuwa Safi.

• Osha Matunda pamoja na mboga za majani kabla ya matumizi

• Hakikisha unapika Nyama Vizuri iive jikoni, hii itasaidia kuua vimelea wote wabaya(harmful germs),

• Hakikisha mazingira ya kupika na kuandaa chakula chako yanakuwa Safi kila wakati.

• Epuka kunywa Maziwa ambayo hayajachemshwa

• Epuka kunywa maji machafu, kunywa maji ya Swimming pool wakati unaogelea, n.k

PIA Kumbuka; Bacteria Wengine unaweza kuwapata kutoka kwa Mwenzako, Watoto n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!