CHANZO CHA KUVIMBA TEZI ZA SHINGONI(Swollen Neck Lymph glands/nodes)
Kuvimba kwa tezi za shingoni(swollen neck lymph glands/Nodes), Tezi hizi hujulikana kama Lymph nodes au Lymph glands, na zinapatikana kwenye maeneo mbali mbali mwilini ikiwemo shingoni,chini ya kidevu,kwapani,sehemu za siri n.k
Tezi hizi za lymph glands hufanya kazi kubwa kwenye kupambana na maambukizi ya magonjwa(Infections) mwilini,
na zinafanya kazi kama filters,zikishikilia au kufanya trapping ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama Bacteria,Virusi n.k kabla havijashambulia sehemu zingine za mwili.
Maeneo makubwa ambayo unaweza kuona tezi hizi za Lymph glands zimevimba ni pamoja na shingoni,chini ya kidevu,kwapani na sehemu za siri.
KUMBUKA; kuvimba kwa tezi hizi za Lymph nodes ni ishara kwamba kuna kitu hakipo sawa mwilini, kama vile mwili umepata infection ya aina yoyote n.k
DALILI HIZI HAPA HUWEZA KUONEKANA KWA MGONJWA
- Kuvimba kwa tezi za shingoni,kwapani,chini ya kidevu au sehemu za siri
- Kupata maumivu kwenye tezi hizi za Lymph nodes
- Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na Homa
- Kuvuja sana jasho wakati wa usiku(Night sweats)
- Wengine hupata Runny nose, pamoja na Sore throat
- Kuvimba kwa tezi hizi karibu sehemu zote za mwili hasa kwa Maambukizi ya magonjwa kama HIV/AIDS,lupus, rheumatoid arthritis,mononucleosis n.k
CHANZO CHA KUVIMBA TEZI ZA SHINGONI(Swollen Neck Lymph glands/nodes)
• Kwa Asilimia kubwa tezi za Lymph nodes huvimba kutokana na maambukizi(Infection) ya Bacteria pamoja na Virusi.
ila mara chache sana kuvimba kwa tezi hizi za lymph glands huweza kutokea kwa mgonjwa wa kansa au Saratani.
• Haya hapa ni maambukizi ambayo kwa asilimia kubwa huweza kupelekea kuvimba kwa tezi hizi
- Maambukizi ya virusi vya ukimwi(HIV/AIDS)
- Uwepo wa Common Cold
- Strep throat
- Maambukizi kwenye sikio(Ear infections)
- Uwepo wa Measles
- Maambukizi kwenye jino-Infected (abscessed) tooth
- Maambukizi kwenye ngozi au kidonda chochote(Skin or wound infections, such as cellulitis)
- Tatizo la Mononucleosis n.k
• Pia mara chache sana maambukizi haya hapa chini huweza kusababisha tezi hiz kuvimba
- Ugonjwa wa Tb(Tuberculosis)
- Baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile kaswende(syphilis)
- Maambukizi ya Parasite kama vile; Toxoplasmosis n.k
- Matatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili kama vile: Tatizo la Lupus,Rheumatoid arthritis n.k
- Uwepo wa Saratani(Cancers) kama vile;Lymphoma,Leukemia N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!