Ticker

6/recent/ticker-posts

Dalili za Ugonjwa wa CHEMBE YA MOYO,Soma hapa



Dalili za Ugonjwa wa CHEMBE YA MOYO,Soma hapa

UGONJWA WA CHEMBE YA MOYO(chanzo,dalili na tiba yake)

Ugonjwa wa chembe ya moyo au kwa kitaalam huitwa angina pectoris ni ugonjwa wa moyo ambao huhusisha maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K

CHANZO CHA UGONJWA WA CHEMBE YA MOYO

Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa chembe ya moyo(angina pectoris), ni kutokana na shida kwenye mishipa ya damu ya moyo hali ambayo hupelekea kuwepo kwa kiwango kidogo cha damu kwenye mishipa ndani ya moyo pamoja na ukosefu wa hewa ya oxygen ya kutosha

Tatizo hili la kwenye mishipa ya moyo huchangiwa na baadhi ya vitu mbali mbali kama vile;

• Ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa kiasi kikubwa sana

• Ulali wa vyakula jamii ya wanga kwa wingi sana

• Matumizi ya pombe kupita kiasi

• Uvutaji wa sigara

• Kupatwa na tatizo la presha

• Uzito kupita kiasi pamoja na unene wa mwili

• Kuwa na tatizo la msongo wa mawazo mara kwa mara

• Kupatwa na hali ya hofu kuu kila mara

• Kuwa na ugonjwa wa kisukari

DALILI ZA UGONJWA WA CHEMBE YA MOYO NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kupata maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K

- Hali ya kushindwa kupumua au kupata shida ya upumuaji

MATIBABU YA UGONJWA WA CHEMBE YA MOYO

Endapo umepata dalili kama hizi ni vizuri kwenda hosptal kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili upate matibabu

VITU VYA KUEPUKA

✓ Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta sana

✓ Epuka uvutaji wa sigara

✓ Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi

✓ Epuka kula vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa

✓ Fanya mazoezi ya mwili wako

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je,chanzo cha Ugonjwa wa chembe ya Moyo ni nini?

Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa chembe ya moyo(angina pectoris), ni kutokana na shida kwenye mishipa ya damu ya moyo hali ambayo hupelekea kuwepo kwa kiwango kidogo cha damu kwenye mishipa ndani ya moyo pamoja na ukosefu wa hewa ya oxygen ya kutosha.

Hitimisho

Ugonjwa wa chembe ya moyo au kwa kitaalam huitwa angina pectoris ni ugonjwa wa moyo ambao huhusisha maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K,

Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa chembe ya moyo(angina pectoris), ni kutokana na shida kwenye mishipa ya damu ya moyo hali ambayo hupelekea kuwepo kwa kiwango kidogo cha damu kwenye mishipa ndani ya moyo pamoja na ukosefu wa hewa ya oxygen ya kutosha.

Ugonjwa wa chembe ya Moyo huweza kuhusisha dalili mbali mbali ikiwemo;

Mgonjwa kupata maumivu makali ya upande wa kushoto mwa kifua na wakati mwingine maumivu haya husambaa hadi mashavuni,shingoni, mgongoni,mkono wa kushoto N.K

- Hali ya kushindwa kupumua au kupata shida ya upumuaji n.k

Ukiona dalili kama hizi hakikisha unapata Msaada Mapema.

 KWA USHAURI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments