Ticker

6/recent/ticker-posts

Dalili za Ugonjwa wa Polio,Soma Zaidi hapa



UGONJWA WA KUPOOZA-UGONJWA WA POLIO-Poliomyelitis(KUPOOZA MIGUU)

Dalili za Ugonjwa wa Polio,Soma Zaidi hapa

POLIO ni ugonjwa wa kupooza ambao upo kwenye kundi la High Infectious Viral Disease, Ugonjwa huu huwapata sana Watoto wenye umri wa chini ya MIAKA MITANO(5),

Virusi wa Polio huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa Mwingine kwa njia ya Faecal-Oral pamoja na njia nyingine kama vile Contaminated water or Food.

Baada ya virusi hawa kuingia kwa njia ya mdomoni,moja kwa moja huanza kuzaliana sana kwenye Utumbo, na hapo ndipo huanza kusambaa maeneo mengine kama vile kwenye mfumo wa fahamu(Nervous system) na kusababisha tatizo la Kupooza(Paralysis) n.k.

DALILI ZA UGONJWA WA POLIO NI PAMOJA NA;

- Joto la mwili kuwa juu sana au kuwa na homa

- Uchovu wa mwili kupita kiasi

- Maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

- Kupata shida ya kichefuchefu pamoja na Kutapika

- Kupatwa na shida ya Sore throat

- Shingo kukakamaa(neck stiffness)

- Maumivu ya Miguu

- Misuli ya mwili kuwa dhaifu sana

- Tatizo la kupooza kabsa hasa miguuni, kisha kumsababishia mtu ulemavu wa kudumu.(Ulemavu wa maisha).

MATIBABU YA UGONJWA WA POLIO

Mpaka sasa hakuna tiba yoyote ya kutibu kabsa ugonjwa huu wa Polio, Ila kuna CHANJO ya kuzuia ili mtu asipatwe na ugonjwa huu mbaya wa Polio.

Ndyo maana Wataalam wa afya tunasisitiza kwa nguvu zote watoto wote chini ya miaka 5 Wawe wameshapata chanjo hii.



Post a Comment

0 Comments