Dalili za Utapiamlo - Jinsi ya Kutambua na Kuzuia

Dalili za Utapiamlo - Jinsi ya Kutambua na Kuzuia

Utapiamlo ni tatizo ambalo linaweza kutokea kwa mtu yeyote, hasa ikiwa hapati lishe bora na inayofaa kwa mwili wake. Dalili za utapiamlo ni ishara kwamba mwili unakosa virutubisho muhimu na kwa hivyo tatizo hili, linapaswa kushughulikiwa mara moja. Makala hii inaelezea dalili za utapiamlo na jinsi ya kuzuia hali hiyo.

Dalili za Utapiamlo

Dalili za utapiamlo hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, lakini hapa kuna baadhi ya dalili ambazo hutokea mara nyingi:

  1. Kupungua kwa uzito kwa kasi
  2. Kuharibika kwa kucha na nywele
  3. Ngozi kuwa kavu na inayochubuka
  4. Upungufu wa nguvu mwilini
  5. Upungufu wa kinga mwilini
  6. Kupungua kwa uwezo wa kufikiria na kujifunza
  7. Kuchelewa kwa maendeleo ya Ukuaji kwa watoto au watoto kudumaa n.k

Jinsi ya Kutambua Dalili za Utapiamlo

Kutambua dalili za utapiamlo ni muhimu ili kuweza kuzuia hali hii hatari. Hapa kuna mambo machache ya kuzingatia:

✓ Pima uzito wa mwili wako kwa kipimo cha uzito mara kwa mara.

✓ Angalia ngozi yako na kucha zako kama zimeharibika au zina kasoro.

✓ Kagua afya ya meno yako na uone kama una dalili za upungufu wa virutubisho.

✓ Pima kiwango cha damu pamoja na upungufu wa virutubisho.

Njia za Kuzuia Utapiamlo

Kuzuia utapiamlo ni muhimu sana ili kuepuka hatari ya kiafya. Hapa kuna njia kadhaa za kuzuia utapiamlo:

- Kula lishe bora yenye mchanganyiko wa vyakula vya protini, wanga, mafuta na mboga mboga.

- Kunywa maji ya kutosha.

- Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi.

- Pata ushauri wa kitaalamu wa lishe ili kufahamu lishe bora zaidi kwa mwili wako.

Jinsi ya Kutibu Utapiamlo

Ikiwa utagundua dalili za utapiamlo, unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu, Ila kwa ujumla hapa kuna njia kadhaa za kutibu utapiamlo:

• Kula chakula chenye virutubisho vyote muhimu kulingana na ushauri wa mtaalamu wa lishe.

• Pata virutubisho vya ziada kwa kushauriwa na daktari wako.

• Kula vyakula vya kusaidia kuongeza uzito kwa ushauri wa mtaalamu wa lishe.

• Fanya mazoezi kwa ushauri wa daktari wako.n.k

Hitimisho

Utapiamlo ni hatari na unapaswa kutibiwa mara moja unapogundulika. Kutambua dalili za utapiamlo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia hali hii hatari.

Kula lishe bora, kunywa maji ya kutosha, kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi na kupata ushauri wa kitaalamu wa lishe ni njia za kuzuia utapiamlo.

Ikiwa tayari una dalili za utapiamlo, unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu kwa ushauri na matibabu sahihi. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuepuka hatari za kiafya zinazotokana na utapiamlo na kuishi maisha yenye afya bora.

Dalili za utapiamlo,Soma hapa Zaidi

Tatizo la Utapiamlo,Chanzo,Dalili na Tiba Yake(Malnutrition)

Tatizo hili huhusisha mtu kutokupata Virutubisho vyote kwa Kiwango Sahihi kinachohitajika mwilini,

ambapo mtu huweza kupata Virutubisho Muhimu kwa kiwango kidogo sana au kwa Kiwango kikubwa kupita Kiasi.

Kwa maana hyo basi, hapa tuna Vitu viwili

Undernutrition: Ambapo Virutubisho vikiwa kwa kiwango kidogo sana

Au Overnutrition: Ambapo Virutubisho vikiwa kwa kiwango kikubwa kupita kiasi.

Dalili hutofautiana lakini mara nyingi huhusisha kupungua uzito, kupungua kwa hamu ya kula, uchovu, n.k

Sababu mbali mbali huweza kuchangia tatizo hili la Utapiamlo kama vile; Kutokula vyakula vyenye virutubisho vyote vinavyohitajika, hali ya kipato kuwa duni, n.k

(1) Undernutrition ni aina mojawapo ya utapiamlo. Hutokea wakati mwili haupati chakula cha kutosha na virutubisho muhimu vya kutosha.

Na Inaweza kusababisha:

  •  Ukuaji kuchelewa au mtoto kudumaa
  • Kuwa na uzito mdogo
  •  Kuwa na shida ya Wasting n.k

Ikiwa mtu hatapata uwiano sahihi wa virutubisho, anaweza kuwa na utapiamlo.

Na inawezekana kuwa na tatizo la Obesity na utapiamlo Kwa Pamoja.

Wakati mtu ana chakula kidogo sana, mlo mdogo, au hali ambayo inazuia mwili wake kupata uwiano sahihi wa virutubisho, inaweza kuathiri vibaya afya yake. Katika hali nyingine, hii inaweza kuwa tishio kwa maisha yake.

(2) Overnutrition

Overnutrition ni aina nyingine ya utapiamlo. Na inatokea wakati mtu anapata virutubisho vingi zaidi kuliko anavyohitaji,

Matokeo yake yanaweza kuwa mkusanyiko wa mafuta mengi mwilini kutokana na virutubisho kupita kiasi, na kusababisha tatizo la uzito kupita kiasi au unene kupita kiasi(Overweight/Obesity).

Kupata virutubisho kupita kiasi kuna athari kadhaa za kiafya, Watu walio na uzito kupita kiasi au wanene wako katika hatari kubwa ya kupata:

  •  ugonjwa wa moyo
  •  shinikizo la damu
  • Tatizo la kisukari
  • Kupata saratani mbali mbali
  • cholesterol kuwa juu n.k

Kiwango cha lishe kupita kiasi kinaongezeka duniani kote. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linaripoti kwamba mwaka wa 2020, asilimia 5.7% ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 walikuwa na uzito uliopitiliza, ongezeko kutoka asilimia 5.4% mwaka wa 2000.

TATIZO LA UTAPIAMLO HUWEZA KUSABABISHA MADHARA MBALI MBALI ikiwemo

- Mtoto kushindwa kukua au kudumaa

- Kinga Mwili kuwa dhaifu sana

- Kushambuliwa na magonjwa mengine kwa Urahisi zaidi

- Ukosefu wa Virutubisho muhimu mwilini kama vile Vitamins n.k

- Vidonda kuchukua Muda mrefu kupona N.k

KUMBUKA- Pia tatizo la Utapiamlo ni Miongoni mwa Sababu Kubwa ya VIFO kwa Watoto wadogo

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA UTAPIAMLO

  • Wazee
  •  Watoto wadogo hasa chini ya Umri wa Miaka 5
  • Wanaotumia Pombe kupita kiasi,
  • Wasio pata mlo kamili n.k

HIZI HAPA NI BAADHI YA DALILI ZA UTAPIAMLO

• Mtoto kutokukua au Kudumaa

• Uzito kuwa Mdogo zaidi au Kupungua

• Mwili kuchoka kupita kiasi

• Kukosa hamu ya kula chakula

• Kuhisi baridi mara kwa mara

• Kukonda,mafuta kupungua-fat, muscle mass au body tissue

• kuumwa Mara kwa Mara,

• Vidonda kuchukua Muda mrefu kupona n.k

CHANZO CHA TATIZO LA UTAPIAMLO

Kutokupata Mlo wa Kutosha au Lishe Duni, hali ambayo husababisha Mwili kutokupata Virutubisho vya kutosha au kwa kiwango kinachohitajika Mwilini,

Unaweza kupata Tatizo la Utapiamlo kwa Sababu hupati Mlo wenye Virutubisho vya Kutosha au Kwa Sababu Mwili wako unashindwa kufyonza Virutubisho kama inavyotakiwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!