Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu
Genital warts ni moja ya aina ya magonjwa ya zinaa,Takribani watu wote wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kuambukizwa angalau aina moja ya virusi vya human papilloma (HPV),
virusi vinavyosababisha vidonda sehemu za siri au masundosundo, wakati fulani wa maisha yao.
Genital warts huathiri zaidi tishu zenye unyevu unyevu za eneo la sehemu za siri, zinaweza kuonekana kama matuta madogo,
yenye rangi kama nyama au kuwa na mwonekano wa cauliflower(tazama kwenye picha). Katika hali nyingine, warts ni ndogo sana kuonekana.
Lakini pia genital warts huweza kujitokeza kwenye maeneo mengine ya mwili kama vile kwenye vidole vya mikono,viganja vya mikono,
Genital warts pia inaweza kutokea mdomoni au kooni mwa mtu ambaye amefanya ngono kwa njia ya mdomo na mtu aliyeambukizwa.
Kwa Wanawake, genital warts zinaweza kutokea kwenye;
- mashavu ya uke au vulva,
- kuta za uke
- eneo katikati ya uke na njia ya haja kubwa
- Eneo kuzunguka njia ya haja kubwa
- Ndani ya uke, pamoja na mlango wa kizazi au cervix.
Kwa Wanaume, genital warts huweza kutokea kwenye;
- Ncha au shimo la uume,
- Kwenye ngozi ya korodani au scrotum,
- Kwenye eneo la haja kubwa(anus).n.k
Dalili za genital warts
Dalili za genital warts ni pamoja na;
- Kuwa na Uvimbe mdogo, wa rangi kama nyama, kahawia au waridi kwenye sehemu zako za siri
- Umbo la cauliflower linalosababishwa na warts kadhaa hufunga pamoja
- Wakati mwingine Kuwashwa sehemu za siri
- Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana
Vidonda vya sehemu za siri vinaweza kuwa vidogo na tambarare kiasi cha kutoonekana,
Hata hivyo, mara chache sana, warts za sehemu za siri zinaweza kuzidi katika makundi makubwa kwa mtu aliye na mfumo wa kinga uliodhaifu.
Chanzo cha Genital warts
Human papillomavirus (HPV) ndyo virusi ambavyo husababisha tatizo la warts,
Kuna zaidi ya aina 40 za HPV zinazoathiri sehemu za siri.
Genital warts karibu kila mara huenea kwa njia ya kujamiiana, na sio lazima genital warts zionekane ili ueneze maambukizi kwa mwenzi wako ambaye unashiriki naye tendo.
Sababu hatarishi za kupata Genital Warts
Watu wengi wanaofanya ngono huambukizwa virusi vya human papilloma(HPV) sehemu za siri wakati fulani.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa ni pamoja na:
✓ Kufanya ngono bila kinga au kondomu
✓ Kuwa na wapenzi wengi
✓ Baada ya kupata maambukizi mengine ya magonjwa ya zinaa
✓ Kufanya mapenzi na mpenzi ambaye hujui historia yake kwenye ngono
✓ Kuanza kufanya ngono katika umri mdogo
✓ Kuwa na mfumo dhaifu wa kinga mwilini mfano kwa wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI (VVU)
Matatizo yanayotokana na genital warts au virusi vya human papilloma (HPV)
Matatizo yanayotokana na genital warts au virusi vya human papilloma (HPV) ni pamoja na:
1. kupata Saratani.
Saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer) imehusishwa kwa karibu na maambukizi ya HPV sehemu za siri,
Aina fulani za HPV pia huhusishwa na;
- saratani za uke,
- njia ya haja kubwa,
- kwenye uume,
- mdomoni na kooni.
Maambukizi ya HPV sio mara zote husababisha saratani, lakini ni muhimu kwa wanawake kufanya kipimo cha "Pap" mara kwa mara, hasa wale ambao wameambukizwa na aina hatari zaidi za HPV.
2. Matatizo wakati wa ujauzito.
Mara chache wakati wa ujauzito, genital warts zinaweza kuongezeka, na kufanya iwe vigumu wakati wa kukojoa.
genital warts kwenye ukuta wa uke zinaweza kuzuia kuvutika kwa tishu za uke wakati wa kujifungua, warts kubwa kwenye vulva au kwenye uke zinaweza kutoka damu wakati wa kujifungua baada ya kuvutwa zaidi.
Ni mara chache sana, mtoto anayezaliwa na mama mwenye genital warts kuwa na warts kwenye koo. Mtoto anaweza kuhitaji upasuaji ili kuzuia njia ya hewa kuziba.
Jinsi ya Kuzuia genital warts
- Epuka ngono zembe au tumia kinga kama condomu wakati wa tendo
- Epuka kuwa na wapenzi wengi
- Epuka kufanya ngono katika umri mdogo
- Pata chanjo ya kuzuia maambukizi ya human papilloma virus(HPV),
Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinapendekeza chanjo ya HPV kwa wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 11 na 12, ingawa inaweza kutolewa mapema kama umri wa miaka 9.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!