Homa ya Nyanya Dalili zake ni Zipi?(Ugonjwa wa homa ya Nyanya)

Homa ya Nyanya Dalili zake ni Zipi?(Ugonjwa wa homa ya Nyanya)

Kuripotiwa kwa visa vipya nchini India vya ugonjwa wa homa ya nyanya kumeibua hofu ya kuenea kwa Ugonjwa huu wa Homa ya Nyanya katika maeneo mengine duniani.

Je Ugonjwa huu ulianzia wapi?

Kwa Mara ya Kwanza Homa ya Nyanya iligunduliwa nchini India. Mnamo Mei 6, 2022, Wizara ya Afya ya India ilithibitisha kisa cha kwanza katika wilaya ya Kollam.

DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA NYANYA

Dalili za homa hii ni zipi?

Dalili za Ugonjwa huu ni Pamoja na;

- Mtu kuwa na malengelenge makubwa mekundu ya mfanano wa nyanya na vipele.

- Vipele hivi Vikiguswa vinaleta maumivu.

- Dalili nyingine za ugonjwa huo ni pamoja na:

• Mtu kupata uchovu,

• Mtu kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika,

• Mtu kupata tatizo la kuharisha,

• Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa,

• Mtu kupata maumivu ya viungo na mwili kuumwa,

• Pamoja na dalili za kawaida za mafua.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU

Kundi gani lenye hatari zaidi ya kuambukizwa homa hii?

- Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wako katika hatari ya kuambukizwa kwa sababu virusi vinaweza kuenea haraka kwa kugusana kwa karibu, kama vile kugusa sehemu chafu au kinyesi cha watu walioambukizwa, au kula vitu vilivyo na virusi.

Hali ya janga la homa hii kwa sasa duniani

Hadi sasa, kuna angalau kesi 100 za homa ya nyanya nchini India, ambapo 82 ni watoto chini ya umri wa miaka 5. Eneo lililo na mlipuko mkubwa zaidi ni Kerala, ikifuatiwa na Tamil Nadu.

Orissa na Haryana Wakati Wizara ya Afya ya India imethibitisha kuwa ugonjwa huo sio hatari kwa maisha. Na kwa sasa madaktari wanatiba dalili zake tu.

Mapema wiki hii ilitoa miongozo ya kuzuia, kupima na matibabu ya magonjwa kwa majimbo yote. Ikiwa mtu yeyote anashukiwa kuambukizwa, anawekwa karantini kwa siku 5-7 baada ya dalili, na wazazi pia wanahimizwa kuwa waangalifu haswa kwa kufuatilia dalili za watoto wao.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!