Jinsi Ya Kuondoa Uchovu Mwilini

 JINSI YA KUONDOA UCHOVU MWILINI

Hizi hapa ni baadhi ya Tips za kukusaidia kuondoa uchovu mwilini

- Hakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku,

uchovu wa mwili ni mojawapo ya dalili za upungufu wa maji mwilini

- Unaweza pia kula ndizi asubuh husaidia kuondoa uchovu hasa ukitumia na maji

- Kula chakupa chepesi ila kinachoupa mwili wako nguvu

- Pata muda wa kutosha wa kupumzika,unashauriwa kulala angalau masaa 6-8 kiafya, ili kumpumzisha mwili wako,

pia pumzika sehemu safi na yenye utulivu wa hali ya juu

- Unashauriwa kusikiliza nyimbo au mziki laini unaoupenda, mziki ni sehemu muhimu sana kwenye mwili wa binadamu

- Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili

- Kaa sehemu ambapo kuna hewa safi,yakutosha pamoja na mzunguko mzuri wa hewa

- Fanya michezo mbali mbali ambayo unaipenda

- Epuka kuendelea kufanya kazi sana,fanya vitu vyepesi vyepesi kwa muda. n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!