Kifaduro ni ugonjwa gani?(chanzo,dalili na Tiba ya Kifaduro)

Kifaduro ni ugonjwa gani?(chanzo,dalili na Tiba ya Kifaduro)

••••

UGONJWA WA KIFADURO

Huu ni ugonjwa unaohusu mfumo wa hewa ambapo mtu hupata maambukizi ya Bacteria au virusi mfano; virusi vya Parainfluenza ambavyo huleta madhara mbali mbali kama kuvimba kwa Njia ya hewa,Koo N.k.

UTAJUAJE KWAMBA MTU ANA UGONJWA WA KIFADURO

Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo mtu mwenye ugonjwa wa kifaduro huonyesha;

- Sauti ya Mgonjwa kukauka

- Mgonjwa kukohoa mara kwa mara na kwa Sauti kama Ya KUBWEKA

- Kupata maumivu ya kifua na mbavu hasa wkati wa kukohoa

- Mgonjwa kupata shida wakati wa Kupumua

- Mgonjwa kuchoka sana

- Mgonjwa kupata mafua

- Joto la mwili kupanda

- Kichwa kuuma

- Na dalili zingine kama kukosa hamu ya kula,kusikia kichefu chefu, kutapika n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA KIFADURO

Kwa asilimia kubwa Mgonjwa wa kifaduro hupewa dawa jamii ya Steroids za kumeza,ambapo inakuwa Dose moja tu au Dawa jamii ya Epinephrini.

Lakini kabla ya matumizi ya dawa yoyote nenda hosptal kwanza kwa ajili ya vipimo,na matibabu kutoka kwa wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!