Ticker

6/recent/ticker-posts

kiungulia husababishwa na nini,Soma hapa kufahamu



 kiungulia husababishwa na nini

CHANZO CHA TATIZO LA KUPATWA NA KIUNGULIA(Au kwa kitaalam heartburn)

Soma hapa kufahamu kuhusu tatizo la kiungulia Pamoja na chanzo chake.

Tatizo la kiungulia

Tatizo la kiungulia ni tatizo ambalo huwapata watu wengi, wakiwemo wakina mama wajawazito,

Kwa namna moja au nyingine kila mtu kwenye vipindi tofauti vya maisha ni lazima apate Tatizo la kiungulia(heartburn).

Chanzo cha Tatizo la kiungulia

Zipo sababu kadhaa ambazo huchangia mtu kupatwa na tatizo la kiungulia,na miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;

-  Kwa mama mjamzito, Mabadiliko ya vichocheo mwilini ambayo hutokea kipindi cha mimba,

Mabadiliko haya huweza kusababisha tatizo la kiungulia.

Hapa nazumgumzia mabadiliko ya vichocheo mbali mbali mwilini ikiwemo;

  • Vichocheo vya Progestrone
  • pamoja na Relaxin

(i). Uzalishwaji mkubwa wa Kichocheo cha Progestrone kwenye damu kipindi cha ujauzito husababisha chakula kitembee taratibu pamoja na mmeng'enyo wake kwenda taratibu sana.

(ii). Uzalishwaji mkubwa wa kichocheo cha Relaxin kwenye damu kipindi cha ujauzito husababisha njia ya chakula yaani Oesophagus kutanuka,

pamoja na vishikizo vya tumbo kulegea yaani Sphinter,

hali ambayo hupelekea chakula kilichopo tumboni kilichochanganyika na Acid kupanda juu,

Na hapa ndipo husababisha tatizo la kiungulia kikali kwa mama mjamzito

- Kuwa na tatizo la Acid reflux(GERD)

- Kuwa na tatizo la Uzalishwaji wa kiwango kikubwa cha acid tumboni kuliko kawaida,

Hii pia huwez kusababisha Tatizo la kiungulia

- Kula kwa wingi vyakula vyenye acid kali kama Maharage,

Hii pia huweza kupelekea mtu kupata Tatizo la kiungulia.

- kula vyakula vya mafuta mengi, Nyanya N.K,

Vyote hivi kwa namna moja au nyingine huweza kuchangia mtu kupata Tatizo la kiungulia.

- Kunywa pombe kupita kiasi

- Kula chakula na kulala kwa muda huo huo N.K

Hizo ni baadhi ya Sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata Tatizo la kiungulia.

Dalili za Tatizo la kiungulia

DALILI ZA Tatizo la KIUNGULIA NI PAMOJA NA;

- Mtu Kuhisi hali ya kuchomwa inayopanda kifuani

- Kuhisi ladha ya kitu kichungu Mdomoni

- Na mara chache maumivu wakati wa kumeza mate.

Hitimisho

Tatizo la kiungulia linaweza kuwa tatizo la muda mfupi tu kisha kuondoka lenyewe, ingawa kwa wengine tatizo la Kiungulia ni tatizo linalojirudia kila siku,

Tatizo la Kiungulia huweza kuzidi zaidi endapo una matatizo mengine ya kiafya kama vile; Tatizo la Acid reflux, vidonda vya tumbo n.k

Hivo kama una tatizo la Kiungulia ambacho hujirudia kila siku, Hakikisha unaongea na wataalam wa afya kwanza,ili kupata msaada zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments