Maambukizi ya Superbugs,chanzo,na Dalili zake
Superbugs ni mjumuisho wa maambukizi ya bacteria, viruses, parasites pamoja na fangasi ambao wamekuwa sugu kwa dawa nyingi ikiwemo antibiotics n.k
Hivo matumizi ya dawa nyingi yamekuwa hayasaidii kabsa kutibu maambukizi haya, hii hupelekea tatizo la drug-resistance infections.
Mfano wa maambukizi ya superbugs ni resistant bacteria ambao wanasababisha tatizo la pneumonia, UTI-urinary tract infections Pamoja na maambukizi kwenye ngozi.
Tatizo la Drug resistance (antimicrobial resistance) dhidi ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria, viruses, parasites pamoja na fangasi huweza kusababisha wagonjwa kuumwa zaidi,kukosa tiba stahiki, na kupelekea madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha.
MOJA YA NJIA ZA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI HAYA NI PAMOJA NA;
- Kuwa na Tabia ya Kunawa mikono na sabuni,maji safi na yanayotiririka mara kwa mara
- Tumia vitakasa mikono au Sanitizer
- Hakikisha mazingira ya kuandaa chakula chako yanakuwa safi muda wote
- Hakikisha unapika nyama iive vizuri,epuka kula nyama ambayo haijapikwa au kuiva vizuri
- Epuka kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa
- Hakikisha maji ya kunywa yanakuwa Safi na Salama
- Epuka kugusana moja kwa moja ya mtu mwenye dalili za magonjwa kama haya
- Hakikisha unapata Chanjo kwa magonjwa ambayo huzuiwa kwa njia ya chanjo
- Tumia Dawa kwa maelekezo tu kutoka kwa wataalam wa afya, epuka matumizi ya dawa kiholela
- Hata kama unajisikia umepona hakikisha unakamilisha dose ya Dawa ulizoanza
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!