MKOJO KUBAKI BAADA YA KUKOJOA(Postvoid urine residual Volume)
Kwa kawaida mtu baada ya kukojoa kibofu cha mkojo yaani Urinary Bladder kinatakiwa kisibaki na mkojo tena utoke wote,
Japo kubaki na kiwango kidogo sana pia sio tatizo,lakini endapo kiwango kikubwa cha mkojo hubaki kwenye kibofu baada ya kukojoa hadi kufikia hatua ya kuchafua nguo au kujikojolea wakati umemaliza kukojoa hilo ni tatizo linahitaji tiba.
HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA TATIZO HILO;
- Matatizo kwenye kibofu cha mkojo(urinary bladder) au kwenye njia ya mkojo(urinary tract)
- Maambukizi ya Bacteria kwenye Njia ya Mkojo yaani UTI
- Kuziba kwenye Njia ya Mkojo
- Tatizo la kukua kwa tezi dume yaani Enlarged prostate
- Side effects za Baadhi ya Dawa
- Njia ya mkojo kupita kuwa ndogo zaidi(Narrowed urethra)
- Tatizo la Neurogenic bladder
MATOKEO YA TATIZO HILI NI PAMOJA;
1. Mtu kukojoa mara kwa mara au karibu karibu
2. Mkojo kutoka pasipo kujizuia-Urine leakage (incontinence)
3. Maambukizi ya UTI za mara kwa mara
4. Mtu kupatwa na shida nyingine ya kuwa na mawe kwenye kibofu cha mkojo(Bladder stones)
5. Mtu kupatwa na shida nyingine ya Figo kuharibiwa(Kidney damage) N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!