Ticker

6/recent/ticker-posts

Sababu Za Mtu Kukosa Pumzi Na Kushindwa Kupumua



 Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha tatizo la mtu kukosa pumzi,kupumua kwa shida au kushindwa kabsa kupumua, na sababu hizo huweza kuwa za muda mfupi yaani Short-term au za muda mrefu yaani Long-term Causes.

SABABU ZA MTU KUKOSA PUMZI NA KUSHINDWA KUPUMUA NI PAMOJA NA;

1. Mtu kuwa na tatizo la Asthma

2. Mtu kuwa na ugonjwa wa wasiwasi yaani anxiety disorders

3. Tatizo la clot za damu kuingia kwenye mapafu hali ambayo hujulikana kama pulmonary embolism

4. Mtu kupatwa na tatizo la kuvunjika mbavu

5. Kuwa na kiwango kikubwa cha maji kuzunguka moyo

6. Mtu kupatwa na tatizo la kupaliwa

7. Mtu kupatwa na tatizo la shambulio la moyo yaani heart attacks

8. Mtu kupatwa na tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi yaani heart failure

9. Tatizo la mapigo ya moyo kubadilika

10. Mtu kupatwa na tatizo la kuishiwa na damu yaani anemia

11. Mtu kupatwa na tatizo la Pneumonia pamoja na maambukizi mengine kwenye mfumo wa hewa

12. Hali ya mama kuwa mjamzito huweza kuchangia pia tatizo hili la kukosa pumzi pamoja na kupumua kwa shida

13. Tatizo la allergy ambayo imepita kiasi yaani Severe allergic reaction maarufu kama Anaphylaxis

14. Mtu kupatwa na shida ya kuvuja damu nyingi kwa gafla N.k

SABABU ZA MUDA MREFU AMBAZO HUWEZA KUSABABISHA TATIZO LA MTU KUKOSA PUMZI NA KUPUMUA KWA SHIDA NI PAMOJA NA;

- Mtu kuwa na ugonjwa wa Asthma

- Mtu kuwa na tatizo la maji kujaa kwenye mapafu

- Tatizo la chronic obstructive pulmonary diseases(COPD) ikiwemo emphysema

- Tatizo la cells zilizovimba kujikusanya mwilini yaani Sarcoidosis

- Magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwemo congestive heart failure

- Kuvimba kwa tissue pamoja na misuli inayozunguka moyo

- Mtu kupatwa na tatizo la saratani ya mapafu

- Mtu kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa TB yaani Tuberculosis n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments