Tabia Ya Kuweka Ukeni Mawe,Vipipi,Vikokoto,

 TABIA YA KUWEKA UKENI MAWE,VIPIPI,VIKOKOTO,SUKARI NGURU n.k

Wale wanawake wanaopenda kuweka mawe ukeni, kuweka vipipi ukeni, kuweka vikokoto ukeni ,kuweka sukari nguru ukeni na kuweka takataka mbalimbali ukeni,

acheni tabia hizi zina madhara mengi kwa afya yako,

Wengine hushauriwa kuweka ukeni hata wakiwa wajawazito,eti kwa lengo la kuongeza uchungu,

Je unayajua madhara ya kutumia vitu kama hivi ukeni?

Moja ya madhara ni pamoja na;

- Kuharibu kabsa hali ya uke(Nature) ikiwa ni pamoja na PH,

Hii husababisha bacteria kupata nafasi ya kushambulia sehemu zako za siri kwa urahisi zaidi.

- Kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa mbali mbali kama vile;

• Maambukizi ya Fangasi

• Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani PID

PID- Pelvic Inflammatory disease

• Maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI n.k

- Madhara wakati wa kujifungua kama vile;

• Kuchanika kwa njia ya kupitisha mtoto

• Kupasuka kwa kizazi kutokana na baadhi ya dawa kuongeza msukumo mkubwa kuliko kawaida,

hali ambayo huweza kumuweka kwenye hatari zaidi mama anayejifungua

EPUKA TABIA KAMA HIZI

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!