Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD),chanzo,dalili,Tiba

 Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD),chanzo,dalili,Tiba

Tatizo hili hujulikana kwa jina Lingine kama Acid Reflux, tatizo hili hutokea pale ambapo Acid kutoka Tumboni hupanda juu kwenye mrija unaounganisha tumbo na Mdomo yaani esophagus,

Hali hii ya acid kupanda juu kutoka tumboni ndyo huanza kuleta shida mbali mbali.

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

- Mtu kuhisi Kiungulia(heartburn) mara kwa mara, hasa baada ya Kula, ambapo huzidi sana wakati wa Usiku au wakati wowote ukiwa umelala

- Mtu kupata shida ya chakula alichomeza au kinywaji alichokunywa kupanda juu au kurudi mdomoni yaani regurgitation

- Mtu Kupata maumivu ya tumbo juu ya kitovu karibu na mbavu au kupata maumivu ya Kifua(kichomi)

- Mtu kupata shida ya Kumeza Kitu yaani dysphagia

- Mtu kuhisi kama kuna kitu kimebakia Kooni

- Wakati mwingine unaweza kupata kikohozi ambacho hakiishi,hasa kama shida hii ya Acid Reflux hutokea wakati wa Usku

CHANZO CHA TATIZO HILI LA GERD

Tatizo hili hutokea pale ambapo Acid hutoka tumboni na kupanda juu kwenye njia ya chakula Mara kwa mara,

Na wakati mwingine content ambazo sio acid pia huweza kupanda juu kutoka tumboni.

Na hii hutokea Pale ambapo band ya Misuli ya Mrivingo inayojulikana kama (lower esophageal sphincter)
ambayo hufanya kazi ya kufunga na kufungua wakati kitu kikiingia au kutoka tumboni kushindwa kufanya kazi vizuri,

endapo Sphincter hii haifungi na kufunguka kama inavyotakiwa au band ya misuli hii ya Mviringo ambayo inabana sehemu ya juu ya tumbo imekuwa dhaifu,basi huweza kupelekea acid ya tumboni pamoja na vitu vingine kuweza kutoka Tumboni na kupanda Juu.

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA MTU KUPATA TATIZO HILI

1. Mtu kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi(Overweight/Obesity)

2. Mwanamke Kuwa Mjamzito

3. Mtu kuwa na tatizo la tumbo kuchelewa kutoa vitu ikiwemo chakula kwenda sehemu zingine yaani Delayed stomach emptying

4. Uvutaji wa Sigara

5. Mtu kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja

6. Mtu kuchelewa sana kula chakula wakati wa Usku

7. Kula aina ya vyakula kwa kiwango kikubwa sana,mfano vyakula vya mafuta mengi n.k

8. Mtu kunywa Pombe au Kahawa mara kwa mara

9. Kuwa na matatizo ya Connective tissues kama vile scleroderma

10. Matumizi ya baadhi ya Dawa mara kwa mara,mfano Asprin n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Tiba ya tatizo hili huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Antiacids za kuneutralize acid tumboni, kupunguza uzalishwaji wa Acid tumboni au Kuzuia kabsa uzalishwaji wa Acid Tumboni.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!