Tatizo la Hyperactivity,chanzo,dalili pamoja na Tiba yake

Dalili za Tatizo la Hyperactivity pamoja na Tiba yake

Tatizo la Hyperactivity huhusisha hali ya mtu Kuhangaika kupita kiasi, kwa Watu kama vile walimu, waajiri, wazazi,walezi n.k,

Mara nyingi ni vigumu kudhibiti tatizo hili kwa watu walio karibu na mtu ambaye ana shida hii ya kuhangaika kupita kiasi(Hyperactivity).

Na kwa mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na hofu au Wasiwasi kutokana na jinsi anavyokuwa, na kwa jinsi watu wanavyomchukulia kulingana na hali yake

HIZI NI BAADHI YA DALILI ZA MTU MWENYE SHIDA HII YA Hyperactivity

Tabia kwa mtu mwenye shida ya hyperactivity ni pamoja na:

- Mtu kutokutulia,kuwa na harakati za mara kwa mara

- Mtu Kuhangaika kupita kiasi

- Kuwa na tabia ya fujo

- Kuwa na tabia ya msukumo

- kukengeushwa kwa urahisi

Ikiwa unajitahidi kukaa kimya au kuzingatia, unaweza kuendeleza matatizo mengine kama matokeo. Kwa mfano, inaweza:

• kusababisha matatizo shuleni au kazini

• kuharibu mahusiano na marafiki au familia

• kusababisha ajali na majeraha

• kuongeza hatari ya kunywa pombe na matumizi mabaya ya dawa za kulevya

Je, ni ishara gani za kuhangaika hutokea kwa WATOTO?

Watoto walio na shida ya Hyperactivity wanaweza kuwa na shida ya kuzingatia shuleni. Wanaweza pia kuonyesha tabia za msukumo, kama vile:

- kuzungumza nje ya utaratibu,kupayuka n.k

- kughairi mambo

- kupiga wanafunzi wengine

- shida ya kushindwa kukaa kwenye viti vyao

Kwa Watu wazima walio na shida ya Hyperactivity wanaweza:

- Kupata ugumu wa kuzingatia kazini

- ugumu wa kukumbuka majina, nambari, au vipande vya habari

- Pia unaweza kupata wasiwasi au huzuni.

Na wakati mwingine tatizo hili huweza kuhusisha afya ya akili yaani Mental health.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA HYPERACTIVITY

Tatizo la hyperactivity linaweza kusababishwa na hali ya kiakili au ya kimwili. Kwa mfano, hali zinazoathiri mfumo wako wa neva au tezi la Thyroid inaweza kuchangia.

Hizi ni baadhi ya Sababu zinazosababisha;

- Tatizo la ADHD (Attention Deficit Hyperactivity Disorder)

- Tatizo la hyperthyroidism

- Matatizo kwenye Ubongo yaani brain disorders

- Matatizo kwenye mfumo wa Neva yaani nervous system disorders

- Matatizo ya Kisaikolojia yaani psychological disorders

- Matumizi ya Dawa za kulevyia kama vile: cocaine au methamphetamine (meth)

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO HILI/VIPIMO

• Uwepo wa Ishara na Dalili kama nilizozitaja hapo

• Kufanyiwa vipimo mbali mbali kama vile; Vya Damu au Mkojo, kisha kuangalia kiwango cha vichocheo(hormones) mwilini,

mfano kwa mtu mwenye shida ya thyroid hormone imbalance anaweza kuwa na tatizo la hyperactivity. n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, Hivo baada ya Daktari kugundua chanzo husika kwako,ndipo matibabu yataanza,

Ila kwa Ujumla kuna tiba ya Mazoezi ya kufanya kama vile; Cognitive behavioral therapy (CBT), au matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo;

✓ dexmethylphenidate (Focalin)

✓ dextroamphetamine and amphetamine (Adderall)

✓ dextroamphetamine (Dexedrine, Dextrostat)

✓ lisdexamfetamine (Vyvanse)

✓ methylphenidate (Ritalin) N.k

Hivo Ongea na Wataalam wa afya ili kupata Vipimo na Matibabu pia

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!