Tatizo la kizunguzungu husababishwa na nini
Tatizo la kizunguzungu hutokea mara kwa mara kwa watu wengi, na inaweza isiwe shida sana ya kuwa na wasiwasi ila wakati mwingine tatizo la Kizunguzungu ni kiashiria kikubwa na muhimu kwamba kuna tatizo mwilini,
Unaweza kupata Tatizo la kizunguzungu kisha likaondoka lenyewe ndani ya muda mfupi sana, ila endapo unapata Tatizo la kizunguzungu mara kwa mara au kwa kujirudia rudia kwa muda mrefu ni muhimu sana kutafuta msaada wa kitaalam.
Katika Makala hii tutachambua zaidi kuhusu chanzo cha Tatizo la kizunguzungu pamoja na Vitu vya kufanya endapo una tatizo hilo.
Tatizo la kizunguzungu husababishwa na nini?
Zipo Sababu mbali mbali ambazo husababisha Tatizo la kizunguzungu ikiwemo;
1. Tatizo la upungufu wa maji mwilini(dehydration),
Endapo una shida hii ya upungufu wa maji mwilini, moja ya dalili ambayo unaweza kuwa nayo ni pamoja na kupata Tatizo la kizunguzungu.
2. Matumizi ya Pombe, hii pia huweza kusababisha shida ya maumivu ya kichwa(migraine headache) pamoja na Tatizo la kizunguzungu
3. Pia tatizo kwenye Sehemu ya ndani ya Sikio(inner ear),
Kumbuka sehemu hii ndyo huhusika na kuleta uwiano au balance katika ya mwili,
Hivo basi, endapo una tatizo lolote linayoathiri sehemu hii ya ndani ya sikio unaweza kupata matatizo mengine ikiwemo Tatizo la kizunguzungu.
4. Pia matumizi ya baadhi ya Dawa,
Baadhi ya dawa huweza kusababisha Tatizo la kizunguzungu, ikiwemo;
- dawa za presha
- dawa jamii ya muscle relaxants
- antiepileptic drugs
- dawa jamii ya antihistamines n.k
5. Kushuka gafla kwa presha yaani Sudden drop in blood pressure,
Presha kushuka gafla Kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo hata kusimama tu kwa muda mrefu yaani orthostatic hypotension,
Hali hii pia huweza kusababisha Tatizo la kizunguzungu.
6. Matatizo mbali mbali ya moyo kama vile;
- Arrhythmia
- Cardiomyopathy,
- shambulio la moyo(heart attack) n.k
7. Kufanya Mazoezi kupita kiasi,
Hata kama mazoezi ni mazuri kwa afya ya mwili,unashauriwa kufanya kwa kiasi,
Ukifanya mazoezi kupita kiasi unaweza kupata madhara mengine kama vile;
- Tatizo la kizunguzungu.
- Maumivu makali ya kichwa
- Mwanamke kukosa hedhi au hedhi kutokueleweka n.k
8. Tatizo la Upungufu wa Damu mwilini(Anemia)
Hii pia huweza kupelekea Tatizo la kizunguzungu.
9. Damu kuwa nyingi kuliko kawaida,
Hii pia huweza kusababisha Tatizo la kizunguzungu.
10. Tatizo la Sukari kushuka(Hypoglycemia)
11. Tatizo la Anxiety disorders,
12. Shida ya Motion sickness,
kwa wale ambao huugua wakisafiri kww kutumia vyombo mbali mbali vya Usafiri kama vile gari,boat,ndege n.k
kama una shida hii ya motion sickness pia unaweza kupata matatizo kama vile;
- Tatizo la kizunguzungu.
- Kutapika sana
- Kuharisha
- Maumivu makali ya tumbo n.k
13. Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali ikiwemo;
- COVID-19
- Maambukiz kwenye Sikio(Ear infection):
- Ugonjwa wa Malaria, UTI n.k
FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara
Je, Upungufu wa maji mwilini huweza kusababisha Tatizo la kizunguzungu?
Ndyo, Moja ya dalili ambazo unaweza kuzipata kama una shida ya Upungufu wa maji mwilini(dehydration) ni Pamoja na kupata Tatizo la kizunguzungu.
Hitimisho:
Tatizo la kizunguzungu huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo; Upungufu wa maji mwilini,upungufu wa damu,kushuka kwa sukari,maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile Ugonjwa wa Malaria, magonjwa ya Moyo n.k
Hivo kama unapata Tatizo la kizunguzungu mara kwa mara ni muhimu kufanya VIPIMO ili kujua shida ni nini.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!