Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo la kujamba kila wakati,Chanzo chake



 Tatizo la kujamba kila wakati,Chanzo chake

Kujamba sio tatizo ambalo ni serious, na kila mtu anajamba kwa vipindi tofauti, ila kujamba sana au kila wakati huweza kuwa kiashiria kwamba kuna kitu hakipo sawa,


Na kwa asilimia kubwa kujamba sana ni kiashiria Mojawapo kwamba tumbo limejaa Gesi au mfumo mzima wa chakula hali ambayo husababisha mtu kujamba sana na tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama flatulence.


Hivo kama kujamba kila wakati chanzo chake ni tumbo kujaa Gesi au mfumo wa chakula kuwa na gesi, Je chanzo cha kujaa Gesi ni nini?


Kila mtu kwa namna moja au nyingine hupata shida hii ya tumbo kujaa Gesi kwenye vipindi mbali mbali vya maisha.


Katika makala hii utajua zaidi kuhusu chanzo cha tumbo kujaa gesi pamoja na dalili mbali mbali ambazo mtu mwenye shida hii huweza kuzipata.


DALILI ZA TUMBO KUJAA GESI NI PAMOJA NA;


- Gesi kutoka sana kwa njia ya haja kubwa(mtu kujamba mara kwa mara)


- Maumivu ya tumbo mara kwa mara


- Kuhisi kushiba muda wote wakati hujala kitu chochote


- Ukubwa wa tumbo kuongezeka n.k


CHANZO CHA TUMBO KUJAA GESI


• Asilimia kubwa ya watu hupata shida hii ya tumbo kujaa gesi kutoka na vyakula au vinywaji,


vyakula ambavyo huongoza kusababisha shida hii ya tumbo kujaa gesi ni pamoja na MAHARAGE, Viazi, Maziwa.N.k


• Unywaji wa Carbonated beverages kama vile SODA,BIA n.k huweza kusababisha tatizo hili la tumbo kujaa gesi


• Kula kwa haraka haraka sana wakati unakula chakula


• Kuongea wakati unakula chakula, hali ambayo huweza kusababisha hewa nyingi kupita tumboni kupitia mdomoni.


• Matumizi ya Fiber supplements nyingi ambazo zina Psyllium n.k


• Magonjwa ya muda mrefu kwenye utumbo yaani Chronic intestinal diseases kama vile; Diverticulitis n.k


• Uwepo wa tatizo la Vidonda vya Tumbo


• Bacteria kuwa wengi kupita kawaida(bacterial overgrowth) kwenye utumbo mdogo, hali ambayo huweza kusababisha mtu kuharisha,uzito wa mwili kupungua kwa kasi,tumbo kujaa gesi n.k


• Wakati mwingine tatizo la kupata choo kigumu au Constipation huweza kusababisha gesi kushindwa kutoka kwa njia ya haja kubwa hivo kujaa tumboni


• Tatizo la Food intolerances, ambapo mfumo wa umeng'enyaji wa chakula hushindwa kuvunja vunja na kufyoza baadhi ya vyakula kama vile maziwa n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments