Tatizo la kuweweseka, kuona vitu visivyo na uhalisia (hallucinations)
Tatizo la kuweweseka, kuona vitu visivyo na uhalisia (hallucinations)
Unaweza kupata shida ya kuweweseka usiku na kuona vitu visivyo na uhalisia tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama hallucinations.
Hallucinations ni pale unaposikia, kuona, kunusa, kuonja au kuhisi vitu vinavyoonekana kuwa halisi lakini vipo tu akilini mwako,Kwa hali ya kawaida Vitu hivi watu wengine hawavioni.
Pata usaidizi wa kimatibabu ikiwa wewe au mtu mwingine ana tatizo hili la Hallucinations.
Aina za Hallucinations
Unaweza kuwa na hallucinations kama:
- Unasikia Sauti ambazo hakuna mtu mwingine anayesikia
- Kuona vitu,watu,taa,hisia ya kuguswa,vitu kutembea mwilini mwako n.k ambavyo si halisi,
- kuhisi harufu ya vitu ambavyo havipo, kuwa na ladha ya vitu ambavyo unahisi tu havipendezi au ni vya ajabu
- Kuhisi Mwili wako unaruka,kupaa n.k wakati sio kweli.
Chanzo cha tatizo la kuweweseka na kuona vitu visivyo halisi(Hallucinations)
Hallucinations inaweza kusababishwa na hali nyingi tofauti za kiafya zinazoathiri hisia,
Sababu zinazochangia tatizo la hallucinations kwa kiasi kikubwa ni pamoja na:
- Hali ya afya ya akili ikiwemo uwepo wa matatizo kama vile ;
- schizophrenia
- au bipolar disorder
- Matumizi ya dawa za kulevyia
- Matumizi ya Pombe
- Magonjwa kama vile;
- Alzheimer's disease
- Au Parkinson's disease
- Kuwa na matatizo ambayo huathiri hali ya uono wa macho, Kusababisha mabadiliko au kupoteza uwezo wa macho kuona vizuri,
Matatizo kama vile;Charles Bonnet syndrome n.k
- Kuwa na tatizo la wasiwasi sana, huzuni au msiba/kufiwa
- Athari kutokana na matumizi ya baadhi ya dawa(side effects)
- Baada ya upasuaji, dawa za usingizi(anesthesia) n.k
Wakati mwingine hallucinations inaweza kuwa ya muda mfupi. Inaweza kutokea ikiwa una tatizo la kuumwa kipandauso(migraines), joto la mwili kuwa juu sana au tu unapoamka au kulala.
Pia hallucinations inaweza kusababishwa na maambukizi, uvimbe kwenye ubongo au tatizo la kuchanganyikiwa (delirium), hasa kwa watu wazee.
Ni rai yangu kwako kama unatatizo la kuweweseka na kuona vitu visivyo na uhalisia, hakikisha unapata msaada haraka.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!