Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo La Mabaka Yanayowasha Chini Ya Matiti



TATIZO LA MABAKA YANAYOWASHA CHINI YA MATITI

Tatizo hili linaweza mpata mwanamke au mtu yoyote lakini limeonekana zaidi kwa wanawake wanene, wale wenye matiti makubwa,wenye kisukari na wale ambao hufanya mazoezi sana au wenye pirikapirika nyingi.

Sababu kubwa ya tatizo hili ni msuguano unaotokana pale sehemu mbili za mwili zinazoangaliana kuwa pamoja.

Msuguano huu uchangiwa na unyevu unyevu (hutokanao na jasho) na hali hii hupelekea michubuko na inflamesheni katika eneo hilo.

Kadri msuguano unavyoongezeka hupelekea michubuko/mpasuko wa ngozi katika eneo hilo (chini ya matiti) na hii hufanyika njia ya bakteria na fangasi kupita na kuingia.

Iwapo fangasi wataingia na kuweka makazi yao hapo basi hupelekea muwasho chini ya matiti na kwa baadhi ya watu hupelekea uchafu mweupe wenye harufu kali/mbaya sanaaa.

Hakikisha unasafisha matiti yako vizuri na kuyakausha vizuri. Vaa nguo zinazozuia misuguano na zinazozuia unyevu unyevu. (Bra za pamba zinafaa zaidi).

Pia unaweza tumia mchanganyiko wa dawa za kupaka ili kuondoa maambukizi ya bakteria na fangasi lakini pia kuondoa hayo mabaka mabaka yatokanayo na inflamesheni. Na iwapo tatizo litaisha unaweza tumia dawa za kupaka za kupunguza utokwaji wa jasho eneo hilo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments