Ugonjwa wa baridi yabisi,chanzo,dalili na Tiba yake
Baridi Yabisi ni ugonjwa unaoshambulia membreni za synovial katika viungo vya binadamu na mara zote hupenda kushambulia sana viungo vidogo na zaidi ya kiungo kimoja na mara zote hupenda kushambulia viungo vya pande zote mbili kwa pamoja(symmetrical).
Ni ugonjwa unaosumbua sana na huweza kumletea mtu madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa viungo na ulemavu mkubwa kama hautatibiwa,
Baridi yabisi yaweza kumpata mtu yeyote katika umri wowote lakini kijinsia ugonjwa huu huwata sanasana wanawake na huanza kuonekana kuanzia miaka 40 na kuendelea kwa walio wengi.
KINACHOSABABISHA BARIDI YABISI
Hakuna Sababu ya moja kwa moja inayosababisha ugonjwa huu; ila zipo tu sababu za kimazingira,kimaumbile,kivinasaba,kifamilia na kijiografia ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa huu.
WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA BARIDI YABISI
1)Wanawake(kwa sababu ya vichocheo vya oestrogen)
2) Wenye Mimba
3) Wasionyonyesha kwa muda mrefu(chini ya mwaka 1)
4) Wanaume wenye upungufu wa kichocheo Testosterone
5) Unene ulopitiliza
6) Wanaovuta sigara
7) Kua kwenye familia yenye watu wenye baridi yabisi.
8) wanaofanya kazi migodini,sheli,wajenzi na viwandani
DALILI ZA UGONJWA WA BARIDI YABISI
Dalili za ugonjwa huu huanza kidogokidogo na kama mtu hataenda kupimwa hospitali unaweza kusema ni mabadiliko ya kawaida,kama mnakumbuka huko juu nilisema matokeo ya ugonjwa huu yaweza kuchukua hadi miaka 20 kuja kukufanya ushindwe kufanya jambo lolote.
Mtu mwenye ugonjwa huu anaanza kupata shida kwenye viungo na baadae mwili mzima hupata matokeo/madhara ya ugonjwa huu..Mgonjwa wa ugonjwa huu anaweza kujikuta anashindwa kufanya yafuatayo bila ya hata yeye kujua ana shida gani;mambo hayo ni kushindwa kufanya shughuli zako za kila siku kama vile;
- KUVAA,
- KUFUNGUA MFUNIKO WA CHUPA,
- KUJISAFISHA UKIWA CHOONI,
- KUTEMBEA,
- KUPANDA NGAZI,
- KUAMKA KUTOKA KWENYE KITI,
- KUFUNGUA MLANGO,
- KUANDIKA,KUCHAPA n.k
DALILI ZA BARIDI YABISI NI KAMA IFUATAVYO;
1. MAUMIVU YA VIUNGO; Mgonjwa wa rheumatoid atapata maumivu ya viungo na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili.. hii yaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu
2. VIUNGO KUKAKAMAA (STIFFNESS):Mgonjwa wa rheumatoid atapata ukakamavu wa viungo kushindwa kufanya kazi zake katika viungo vya mikono; mara zote mgonjwahupata hali hii lile lisaa la kwanza kabisa punde anapoamka na akishamaliza lisaa limoja na kadiri anaendelea kutembea tembea basi hali hio ya ukakamavu wa viungo hupungua.Mgonjwa anaweza kutumia lisaa au zaidi kutoka kitandani….hali hii huonekana katika ugonjwa wa baridi yabisi pekee
3. KUVIMBA VIUNGO; ; Mgonjwa wa rheumatoid viungo vyake vitavimba na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili.. hii yaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu
4. Dalili Zingine ni pamoja na;
- Mwili Kupata Joto(fever)
- Kupungua Uzito(weight Loss)
- Kuchoka Mwili Mzima(chronic Fatigue) n.k
MATOKEO YA BARIDI YABISI KWA MWILI
Ugonjwa huu ni wa viungo lakini unaweza kuleta madhara katika mwili mzima (extra-articular),kwa maana ugonjwa unaweza kutoka nje ya viungo na kuleta madhara katika mfumo wowote katika mwili wa mgonjwa..Sio kila mgonjwa wa rheumatoid atapata madhara ya mwili mzima bali kuna baadhi ambao wapo kwenye uhatari zaidi wa kupata matokeo hayo,baadhi ya walio hatarini ni wenye umri mkubwa,wanaovuta sigara,mwanamke,wenye uharibifu wa viungo,wenye kipimo cha rheumatoid factor POSITIVE. .
Matokeo ama madhara ya rheumatoid katika mwili mzima ni kama ifuatavyo
• Udhaifu Wa Mifupa(osteopenia)
• Udhaifu Wa Misuli(muscle Weakness)
• Mwili Kujaa Mafuta(sarcopenia)
• Manundu Kwenye Ngozi(rheumatoid Nodules)
• Madonda Kwenye Ngozi(skin Ulcers)
• Kua Na Macho Makavu(Keratoconjuctivitis Sicca)
• Matatizo Ya Kupumua
• Magonjwa Ya Moyo
• Matatizo Ya Mishipa Ya Damu(Vasculitis)
• Matatizo Ya Mafigo
• Kiharusi
• Upungufu Wa Damu
NAMNA UGONJWA HUU HUGUNDULIKA
Ugonjwa huu hugundulika tu kirahisi pale unapomuona mtaalam wa afya ,atrakusikiliza juu ya historia ya unavojisikia,atakuchunguza viungo vyako na utafanyiwa vipimo kadhaa vya kubaibini tatizopamoja na kujua kama kuna mdahara ya ugonjwa ulio nao.. Viko vipimo vya damu na vya mionzi katika uchunguzi wa tatizo hili
BARIDI YABISI KWA WAJAWAZITO
Ugonjwa huu kama nilivosema hapo awali huwapata sana wanawake na hasa walio katika umri wa kupata watoto, baridi yabisi kwa wajawazito imekua ni changamoto kwa wataalamu kimatibabu kutokana na hali ya ugonjwa wenyewe na adhari za madawa ya ugonjwa huu kwa wajawazito.
Habari Njema Ni Kwamba Wajawazito Walio Wengi Wenye Ugonjwa Huu Huanza Kujisikia Vizuri Na Hata Dalili Kupotea Zote Kipindi Cha Ujauzito Na Kuanza Kujitokeza Tena Baada Ya Kujifungua.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!