UGONJWA WA BULLOUS PEMPHIGOID NI UGONJWA GANI?
Ugonjwa huu unaitwa Bullous pemphigoid,
ni ugonjwa ambao unapelekea ngozi kua na malenge lenge makubwa ambayo hutokea sana sana maeneo mbali mbali ya mwili kama vile;
ya mgongoni,kifuani,miguu na mikono hasa kwenye mikunjo,makwapani na mudomoni.
ugonjwa huu ni mojawapo ya magonjwa yatokanayo na mwili kujishambulia wenyewe(autoantibody-mediated damage to epithelial basement membrane zone),
japokua bado haijulikani vizuri namna ushambuliaji hua unavyotendeka au kutokea.
Ugonjwa huu unaweza kuonekana sana kama mtu ana tatizo la aleji ,au kama ana maambukizi ya vimelea kama vya homa ya ini(hepatitis B, hepatitis C), Helicobacter pylori, cytomegalovirus Toxoplasma gondii na HIV.
Tatizo hili lina matibabu yake ili kupunguza utengenezwaji wa malengelenge,
kumuondolea mtu adha ya miwasho miwasho,kumuondolea mtu stress itokanayo na kuharibika ngozi nk,
ziko dawa za kupaka na kumeza ambazo mtu anaweza kutumia hadi kwa miezi 3 au 6
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!