UGONJWA WA GUILLAIN-BARRE SYNDROME,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Guillain-Barre syndrome huu ni ugonjwa ambao hutokea mara chache sana na ugonjwa huu huhusisha Mfumo wa kinga ya mwili yaani Body immunity system kushambulia mfumo wa fahamu au Nerves zako mwilini.
DALILI ZA UGONJWA WA GUILLAIN-BARRE SYNDROME
Ugonjwa huu huhusisha dalili pamoja na Ishara mbali mbali ikiwa ni pamoja na;
1. Misuli ya mwili kuanza kudhoofika na kukosa nguvu kabsa,na udhaifu huu huanzia kwenye misuli ya miguuni kisha kusambaa kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama Mikononi n.k
2. Mtu kuhisi hali ya kuchomwa na kitu cha ncha kali kama sindano kwenye vidole vya miguuni,mikononi,kwenye kisigino cha mguuni n.k
3. Mtu kutembea kwa shida,kushindwa kutembea kabsa au kushindwa kupanda ngazi sehemu ambapo kuna ngazi
4. Mtu kupata shida ya kuongea,kushindwa kutafuna au kumeza kitu chochote
5. Mtu kupata shida ya kuona au kuona marue rue yaani double vision
6. Kupata maumivu makali ya viungo mbali mbali vya mwili hasa wakati wa usiku
7. Mtu Kushindwa kudhibiti utendaji kazi wa kibofu chake cha mkojo, hali ambayo huweza kusababisha matatizo kama kujikojolea n.k
8. Mtu kupata tatizo la Mapigo ya moyo kwenda mbio
9. Mtu Kuwa na tatizo la Presha kushuka au kupanda
10. Mtu kupata shida sana wakati wa upumuaji n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME
Mpaka sasa chanzo cha moja kwa moja dhidi ya ugonjwa huu hakijajulikana, ila kuna baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili na sababu hizo ni kama vile;
- Kuwa na umri mkubwa lakini pia tafiti zinaonyesha ugonjwa huu hushambulia wanaume zaidi ya wanawake
- Mtu kushambuliwa na bacteria anayejulikana kwa jina la campylobacter,bacteria huyu hupatikana kwenye nyama ya kuku ambayo haijaiva vizuri
- Mtu kushambuliwa na virusi mbali mbali kama vile; Virusi vya mafua yaani Influenza virus,Cytomegalovirus,Epstein-Barr virus,Zika virus n.k
- Mashambulizi ya homa ya Ini Kama vile HEPATITIS A,B,C na E
- Maambukizi ya virusi vya ukimwi yaani HIV/AIDS
- Mtu kupatwa na ugonjwa wa Pneumonia kama vile Mycoplasma pneumonia n.k
- Mtu kufanyiwa upasuaji wa aina mbali mbali mwilini
- Mtu kupata ajali au kuumia pamoja na kupatwa na matatizo mengine kama vile Hodgkin's lymphoma n.k
MADHARA YA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME
kama nilivyokwisha kuelezea hapo mwanzo kwamba tatizo hili huhusisha mfumo wa kinga ya mwili kushambulia NERVES zako mwilini,hivo moja kwa moja mgonjwa hupata madhara yanayotokana na uharibifu wa Nerves mwilini kama vile;
• Kupumua kwa shida au kupata shida ya upumuaji
• Misuli ya mwili kuwa dhoofu hasa miguuni na kupelekea mtu kushindwa kutembea n.k
• Mtu kuhisi hali ya kuchomwa na kitu cha ncha kali kama sindano kwenye vidole vya miguuni,mikononi,kwenye visigino n.k
• Mtu kuanza kuwa na matatizo ya Presha au shinikizo la damu
• Mtu kuanza kuwa na matatizo mbali mbali ya moyo
• Mtu kuhisi maumivu makali ya viungo
• Mtu kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo
• Mtu kuanza kupata tatizo la damu kuganda au kutengeneza clots,kuwa na vidonda yaani Pressure sores hii ni kutokana na mtu kulala kwa muda mrefu au kutokuwa na uwezo wa kutembea mara kwa mara
MATIBABU YA TATIZO HILI LA GUILLAIN-BARRE SYNDROME
Hakuna tiba ya kuondoa kabsa tatizo hili,ila kuna matibabu ya kudhibiti dalili zinazotokana na tatizo hili na kumsaidia mgonjwa kurecover kama mwanzoni ingawa bado tatizo analo mwilini mwake, na matibabu hayo ni kama vile;
✓ Tiba ya Plasma exchange yaani plasmapheresis
✓Huduma ya Immunoglobulin therapy, ambapo mgonjwa hupewa Immunoglobulin ambazo zina Antibodies salama yaani healthy antibodies kutoka kwa mtu aliyemchangia damu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!