UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO(MENINGITIS),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Homa ya uti wa mgongo kwa kitaalam hujulikana kama meningitis, ni tatizo ambalo huhusisha maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye sehemu kuu mbili ubongo pamoja na Uti wa mgongo.
Homa ya uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa,soma hapa chini kujua visababishi vya tatizo la homa ya uti wa mgongo.
VISABABISHI VYA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;
1. Maambukizi ya Bakteria mbali mbali kama vile; Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae na Mycobacteria tuberculosis
2. Maambukizi ya Virus mbali mbali kama vile; Herpes simplex type 2, HIV na Varicella zoster.
3. Maambukizi ya Fangasi mbali mbali kama vile; Coccoidiodomycosis na Cryptococci meningetides.N.k
DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;
1•Shingo kukakamaa na kuwa ngumu isivyo kawaida
2•Mgonjwa kujihisi homa kali au joto la mwili kuwa juu sana
3•Mgonjwa kupata Maumivu makali sana ya kichwa
4•Mgonjwa kupoteza fahamu au uwezo wa kukumbuka vitu
5•Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa
6•Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)
7•Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)
8•Kwa watoto, kuvimba utosi n.k
MADHARA YA TATIZO HILI LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;
1•Kuamshwa kwa chembechembe za damu zinazo sababisha damu kuganda kitaalamu hujulikana kama – Disseminated Intravascular Coagulopathy (DIC).
2•Kuvuja damu katika tezi za adrenalin na kupelekea kutokea kwa ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa – waterhouse friderichsen syndrome.
3•Kwa watoto, ugonjwa huu unaweza kusababisha mtoto kuwa na kichwa kikubwa - hydrocephalus pamoja na madhara mengine.
MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO
Kwa wagonjwa waliopoteza fahamu ni vizuri kuhakikisha wanapumua vizuri, na njia za hewa ziko wazi. Halikadhalika, iwapo itathibitika kuwa bakteria ndiyo wanaosababisha ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kupewa mojawapo ya dawa hizi za antibiotiki kama cefotaxime au Cefriaxone. Aidha baadhi ya madaktari hupendelea kuongeza dawa za steroids kama dexamethasone kama sehemu ya matibabu.
Iwapo itathibitika ugonjwa huu umesababishwa na virus, dawa kama Acyclovir huweza kutumika. Hali kadhalika, ikithibitika kuwa vimelea waliosababisha ugonjwa huu ni wa kundi la fungus, dawa kama Amphotericin B au flucytosine zaweza kutumika. Mgonjwa pia hupewa Paracetamol kwa ajili ya kushusha homa na kuondoa maumivu ya kichwa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!