Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa Leptospirosis au Homa ya Mgunda,chanzo,Dalili na Tiba yake



Ugonjwa wa Leptospirosis au Homa ya Mgunda,chanzo,Dalili na Tiba yake

Ugonjwa huu wa leptospirosis au Homa ya Mgunda ni miongoni mwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa Binadamu na unasababishwa na Bakteria aina ya Leptospira interrogans.

Ugonjwa huu umekuwepo katika maeneo ya kitropiki ambayo ni yenye hali ya joto katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na Australia,

Wanyama aina za panya, kindi, mbweha, kulungu, swala, na wanyamapori wengine wameripotiwa kupata maambukizi ya vimelea hivi na kuwa chanzo cha maambukizi kwa Binadamu”

Ugonjwa wa Homa ya Mgunda huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa Binadamu kupitia uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji,kutoka katika mkojo wa wanyama wenye maambukizi.

FAHAMU KWAMBA;Leptospirosis ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria, unaoathiri wanadamu na wanyama, Bakteria hawa wapo kwenye genus ya Leptospira na wanaweza kupita kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu kupitia vidonda, vinapogusana na maji au udongo ambapo mkojo wa wanyama upo.

Aina kadhaa za bakteria wa Leptospira  husababisha leptospirosis.

Bakteria hawa wanaweza kuingia ndani ya mwili kupitia majeraha ya wazi, macho, au utando wa mucous. Wanyama wanaoambukiza wanadamu ni pamoja na panya,mbweha, mbwa, popo, kondoo, farasi, ng'ombe, nyati na nguruwe.

NJIA ZA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA HOMA YA MGUNDA,

Hizi hapa ni baadhi ya njia za maambukizi ambapo mtu huweza kupata Ugonjwa huu wa Homa ya Mgunda,

1. Kugusa mkojo (au maji maji mengine ya mwili) kutoka kwa wanyama wenye maambukizi.

2. Kugusa maji, udongo, au chakula kilichochafuliwa na mkojo wa wanyama wenye maambukizi.

3. Kunywa maji yaliyochafuliwa na vimelea vya
bakteria wa ugonjwa huu

KUNA AINA MBILI KUU ZA LEPTOSPIROSIS

1.Leptospirosis isiyo kali(Mild leptospirosis): Dalili ni pamoja na maumivu ya misuli, baridi, maumivu ya kichwa n.k

2. Leptospirosis kali(Severe Leptospirosis): Hii huweza kusababisha Kushindwa kwa viungo, kuvuja damu puani na maeneo mengine, hata kusababisha kifo ikiwa bakteria wameambukiza ini, figo, na viungo vingine vikuu.

DALILI ZA UGONJWA HUU WA LEPTOSPIROSIS

Ishara na dalili za leptospirosis kwa kawaida huonekana ghafla, takribani siku 5 hadi 14 baada ya kuambukizwa, Hata hivyo, kipindi cha incubation kinaweza kuanzia siku 2 hadi 30, kulingana na CDC.

(1) DALILI ZA MILD LEPTOSPIROSIS(Nyepesi au Isiyokali)

Ishara na dalili za leptospirosis isiyo kali ni pamoja na:

- homa na baridi

- kukohoa

- kuhara, kutapika, au vyote viwili

- maumivu ya kichwa

- maumivu ya misuli, haswa chini ya mgongo na eneo la Calves

- Kuwa na upele au rashes

- macho kuwa mekundu

- Mgonjwa Kupata homa ya manjano au jaundice

Watu wengi hupona ndani ya wiki moja bila matibabu, lakini karibu asilimia 10 huendelea kupata leptospirosis kali.

(2). DALILI ZA SEVERE LEPTOSPIROSIS(Leptospirosis kali)

Ishara na dalili za leptospirosis kali itaonekana siku chache baada ya dalili za leptospirosis isiyokali kutoweka.

Dalili hizi hutegemea ni viungo gani muhimu vinavyohusika. Inaweza kusababisha kushindwa kwa figo au ini,matatizo ya kupumua na homa ya uti wa mgongo. Hizi zinaweza kuwa dalili mbaya zaidi endapo Moyo, ini na figo vimeathirika.

Baadhi ya Dalili za Leptospirosis kali ni pamoja na;

- uchovu wa mwili kupita kiasi

- kuishiwa na nguvu

- mapigo ya moyo kwenda mbio

- maumivu ya misuli

- kichefuchefu

- Mtu kutokwa na damu puani

- maumivu katika kifua

- Kupata shida ya kuhema au kupumua

- Kukosa kabsa hamu ya chakula

- uvimbe wa mikono, miguu, au vifundoni

- kushuka kwa uzito bila sababu

- homa ya manjano, ambayo huonyesha dalili mbali mbali kama vile unjano wa macho, ulimi, na ngozi

Ikiwa ubongo au uti wa mgongo,
vimeathiriwa ugonjwa wa meningitis, encephalitis, au vyote viwili vinaweza kutokea.

Meningitis ni maambukizi yanayohusisha utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo, wakati encephalitis inahusu maambukizi ya tishu za ubongo. Hali zote mbili zina dalili zinazoweza kufanana,ikiwemo:

- Mtu kuchanganyikiwa

- kusinzia

- homa kali

- kichefuchefu

- shingo kuwa ngumu au kukakamaa

- kutokuwa na uwezo wa kuzungumza

- kutapika

- tabia ya fujo au kutokutulia(Restless) n.k

ZINGATIA PIA MAMBO HAYA MUHIMU

• Epuka kunywa maji ya Mto(River water) bila kuyachemsha au kuyatibu

• Dhibiti Panya, na hakikisha wanyama kama Mbwa n.k wanaoshwa kwa dawa mara kwa mara

• Epuka kushika wanyama waliokufa kwa kutumia mikono mitupu, Vaa gloves kwanza

• Hakikisha unanawa mikono na maji safi na Sabuni,

Lakini pia WHO wanasema Hatari ya Ugonjwa huu huweza kuzidi zaidi kipindi cha mvua nyingi(excessive rainfall), pamoja na Mafuriko.



Post a Comment

0 Comments