Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa Lyme,chanzo,dalili na Matibabu yake



Ugonjwa wa Lyme,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Lyme ni ugonjwa unaoenezwa na kupe

Lyme ni mji wa Marekani ambapo mwaka wa 1975 kisa cha kwanza cha ugonjwa unaoitwa 'Lyme disease' kiligunduliwa.

Ugonjwa wa Lyme ni nini?

Ugonjwa wa Lyme au borreliosis ni ugonjwa unaoathiri viungo na sehemu tofauti za mwili, Ugonjwa huu unasababishwa na bakteria: Borrelia, spirochaete ambao hupitishwa kwa binadamu kwa kuumwa na kupe aliyeambukizwa.

Dalili za Ugonjwa wa Lyme

Kwa kuwa ni ugonjwa unaoathiri viungo na sehemu tofauti za mwili, dalili za Ugonjwa wa Lyme zinaweza kuwa tofauti sana na kutofautiana kulingana na hatua ya ugonjwa huo.

Kwa upande wa udhihirisho wa ugonjwa wa Lyme, ugonjwa una 'hatua' 3 tofauti.

✓ Kwa Ujumla, Dalili za Mwanzoni za Ugonjwa wa Lyme ni pamoja na;

  • Kupata homa
  • baridi;
  • Kupata maumivu ya misuli (myalgia);
  • Kupata maumivu ya pamoja (arthralgia);
  • Kupata maumivu ya kichwa;
  • uchovu mkali na udhaifu (asthenia);
  • kuungua na kuwasha kunakosababishwa na mwanga na joto (photophobia)
  • Kuvimba kwa lymph nodes

✓ Ishara na Dalili za Baadaye ( ambazo hutokea kuanzia siku kadhaa hadi miezi baada ya kuumwa na Kupe)

- Kuvimba Goti

- kupata tatizo la Kupooza usoni(Facial Palsy)

- Kupata Maumivu makali ya kichwa na shingo kuwa ngumu au kukakamaa(neck stiffness)

-  Kupata tatizo la Arthritis ambapo huambatana na maumivu makali ya viungo na uvimbe, hasa kwenye magoti na viungo vingine vikubwa.

- Kupata Maumivu ya mara kwa mara kwenye tendons, misuli, viungo, na mifupa

- Mapigo ya moyo kubadilika (Lyme carditis)

- Kuhisi kizunguzungu,kukosa pumzi n.k

- Kupata Uvimbe kwenye Ubongo na Uti wa mgongo(Inflammation of the brain and spinal cord)

- Kupata maumivu kwenye Neva(Nerve pain)

- Kupata Maumivu kama kitu kinakuchoma, kufa ganzi, au kuwashwa kwenye mikono au miguu. n.k

Kwa kawaida Ugonjwa wa Lyme ukiwa kwenye hatua za awali(Stage 1) huwa na dalili kama hizi;

  • Kupata Homa(Fever).
  • Maumivu ya kichwa
  • Uchovu wa mwili kupita kiasi
  • Joints kukakamaa(Joint stiffness).
  • Kupata maumivu ya misuli
  • Pamoja na Kuvimba kwa lymph nodes.

Ugonjwa wa Lyme ukiwa kwenye hatua ya Pili(Stage 2) huwa na dalili kama hizi;

Kama hujapata matibabu, ugonjwa wa Lyme unaweza kuwa mbaya zaidi. Dalili mara nyingi huonekana ndani ya wiki 3 hadi 10 baada ya kuumwa. Hatua ya 2 mara nyingi ni mbaya zaidi na huenea zaidi, Hatua hii Inaitwa "early disseminated disease".

Hatua ya 2 inaweza kujumuisha dalili zifuatazo:

- Kuwa na upele mwingi kwenye sehemu mbali mbali za mwili

- Kupata maumivu ya shingo

- Shingo kukakamaa

- Misuli ya usoni kuwa dhaifu, hali hii huweza kutokea upande mmoja au pande zote mbili za Uso

- Mapigo ya moyo kubadilika(Irregular heartbeats)

- Kuwa na Maumivu ambayo huanza kutoka mgongoni na kwenye nyonga kuenea kwenda miguuni.

- Maumivu, ganzi au udhaifu kwenye mikono au miguu.

- Kuvimba kwenye tishu za jicho au kope ambako huambatana na maumivu.

- Kuwa na maumivu ya macho pamoja na shida ya macho kupoteza uono n.k

Ugonjwa wa Lyme ukiwa kwenye hatua ya tatu(Stage 3) huwa na dalili kama hizi;

Dalili katika hatua hii ni pamoja na arthritis katika viungo vikubwa, hasa magoti. Maumivu, uvimbe au ugumu ambao unaweza kudumu kwa muda mrefu. dalili zinaweza kuja na kuondoka. Dalili za hatua ya 3 kwa kawaida huanza miezi 2 hadi 12 baada ya kuumwa na kupe.

Matibabu ya Ugonjwa wa Lyme

Antibiotics hutumiwa kutibu ugonjwa wa Lyme. Katika hali nyingi, ahueni itakuwa ya haraka zaidi baada ya matibabu ya haraka huanza.

Dawa za Vidonge:

Matibabu ya kawaida ya Ugonjwa wa Lyme ni antibiotic zinzotumika kama vidonge. Matibabu haya kwa kawaida huchukua siku 10 hadi 14. Matibabu yanaweza kuwa ya muda mrefu kulingana na dalili zako. Ni muhimu kumeza dawa zote kama ulivyoelekezwa hata kama unajisikia nafuu.

Dawa za Sindano(IV antibiotic):

Mtoa huduma wako anaweza kuagiza antibiotiki inayotolewa moja kwa moja kwenye mshipa, Dawa ya IV inaweza kutumika kwa ugonjwa ukiwa kwenye hatua ya hatari zaidi, hasa ukiwa una dalili za;

• Arthritis ya muda mrefu.

• Ugonjwa unaoathiri mfumo wa neva.

• Au Ugonjwa unaoathiri moyo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments