Ugonjwa Wa Ocd,Chanzo,Dalili Na Tiba

 UGONJWA WA OCD,CHANZO,DALILI NA TIBA

OCD-hiki ni kifupi cha Obsessive-compulsive disorder,ambapo tunazungumzia ugonjwa wa kisaikolojia

Huu ni ugonjwa wa kisaikolojia ambao unawapata binadamu na kumpelekea binadamu kuwa na mawazo ya kujishtukia shtukia mara kwa mara.

Ugonjwa huu unampelekea mtu kua na mawazo ya kuogopa, kuugua au kuhisi kwamba anaugua ugonjwa fulani na kwa mawazo hayo mtu anakua na tabia ya kujihami hami sana kwa aidha kunawa mikono,kutokusalimiana na watu,kupenda kwenda hospitali mara kwa mara na kuomba kupimwa magonjwa yote na hata kama akikutwa hana ugonjwa bado anaweza kuomba kupewa dawa za ugonjwa anaoufikiria kichwani.

DALILI ZA UGONJWA WA OCD NI PAMOJA NA;

- Mtu kuogopa kujichafua kila mara hali ambayo huweza kupelekea tabia kama vile;kunawa mikono kila dakika

- Mtu kuwa na tabia ya kujishtukia pamoja na kuwa na mashaka na kila kitu

- Mtu kutaka kila kitu kiende kwa utaratibu flani bila kubadilishwa

- Mtu kuwa na hali ya kuona anaendesha gari lake halafu kati kati ya umati mkubwa wa watu

- Wakati mwingine watu wenye ugonjwa wa OCD huwa na mawazo ya kujidhuru wenyewe au kudhuru mtu mwingine

- Mtu kuanza kurudia baadhi ya vifungu vya maneno,maombi n.k

Watu wenye OCD wanakuaga na hofu ya karibia kila kitu,mfano anaweza kuona milango,vitasa,meza zimejaa vijidudu na hivo kua na katabia ka kunawa kila wakati na kumeza vidonge ili kuua hao vimelea.

Ugonjwa huu unatesa sana na mgonjwa anakua na dalili au mitazamo inayojirudia rudia mara kwa mara mfano mgonjwa anaweza kua anakuja hospitali mara kwa mara kwa malalamiko ya kuhisi ana UTI kwa kua anafanya kazi maeneo ya watu wengi au kuhisi ana maambukizi kwenye kifua kwa kua yupo kwa watu wengi,alikua kwenye daladala na kuna mtu alikua anahema vibaya hivo anakua anaomba kutibiwa na antibiotiki.

CHANZO CHA UGONJWA WA OCD

Ugonjwa huu unawapata sana wanaume,unatembea kwa baadhi ya familia. Ugonjwa huu unatokea endapo kukitokea hitilafu kwenye ubongo hasa kwenye sehemu za kuratibu mambo ya tabia ,ujifunzaji wa mambo na ufahamu,sehemu hizo ni sehemu ya ubongo wa mbele na nukliasi za caudate na globus pallidus.

- Mabadiliko kwenye utendaji kazi wa ubongo wako pamoja na biolojia yaani body's own natural chemistry or brain functions.

- Matatizo ya kigenetics au Genes,hali ambayo hupelekea tatizo hili kuwepo kwenye familia flani au koo flani

- Pia shida hii huweza kutokea kwa kujifunza(Learning),ambapo mtu huweza kujifunza kutoka baadhi ya wanafamilia wenye shida hyo n.k

VITU AMBAVYO HUONGEZA UWEZEKANO WA MTU KUPATWA NA UGONJWA HUU WA OCD

- Kuwa na mtu mwenye shida hii kwenye familia yenu huongeza uwezekano wa wengine kupata pia

- Mtu kupatwa na matukio makubwa kwenye maisha yake ambayo huleta msongo zaidi wa mawazo

- Mtu Kuwa na matatizo mengine ya akili kama vile; anxiety disorders, depression, substance abuse or tic disorders.

MATIBABU YA UGONJWA WA OCD

Kwa asilimia kubwa matibabu ya ugonjwa wa OCD huwa kwenye kudhibiti dalili ambazo husababishwa na ugonjwa huu, na hapa tunazungumzia matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;

• Dawa jamii ya Antidepressants mfano;

Clomipramine (Anafranil) kwa watu wazima na watoto wa kuanzia miaka 10

Fluoxetine (Prozac) kwa watu wazima na watoto wa kuanzia miaka  7

Fluvoxamine kwa watu wazima na watoto wa kuanzia miaka  8

Paroxetine (Paxil, Pexeva) kwa watu wazima pekee

Sertraline (Zoloft) kwa watu wazima na watoto wa kuanzia miaka  6 N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!