Ugonjwa wa Rovu,chanzo,Dalili na Tiba yake

 Ugonjwa wa Rovu,chanzo,Dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa Rovu ndyo kwa jina lingine hujulikana kama Goiter,

FAHAMU UGONJWA WA GOITA AU ROVU

Goita (Goiter) Au Rovu ni hali ya kuvimba kwa tezi ya thyroid. Uvimbe huu hautokani na saratani (goita si saratani). Tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo. Kazi kuu za tezi ya thyroid ni kuzalisha homoni mbalimbali ambazo husaidia mwili kuthibiti na kufanya kazi zake mbalimbali.

VIHATARISHI VYA GOITA au ROVU

Kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na kurithi yanayoweza kusababisha mtu kupata goita. Vihatarishi hivi ni pamoja na:

1. Kuwa na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea

2. Historia ya ugonjwa wa goita miongoni mwa wanafamilia

3. Hali ya kuwa mwanamke

4. Na, kutopata iodine ya kutosha katika lishe. Iodine ni madini muhimu yanayohitajika katika utengenezaji wa homoni mbalimbali zinazozalishwa na tezi ya thyroid. Watu wanaoishi kwenye maeneo mbali kutoka pwani ya bahari au yaliyo katika nyanda za juu kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa wapo katika hatari ya kupata goita kwa vile hawapati madini ya kutosha ya Iodine katika chakula chao.

•Soma: Ugonjwa wa Mgongo Wazi kwa Watoto,chanzo,Dalili na Tiba yake

DALILI ZA GOITA AU ROVU NI ZIPI?

Dalili kuu ya goita Au Rovu ni kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi ya thyroid. Ukubwa wa tezi unaweza kuwa kijiuvimbe kidogo katika tezi au uvimbe mkubwa kama nundu sehemu ya mbele ya shingo. Kuvimba kwa tezi ya thyroid kunaweza kusababisha mgandamizo katika njia ya hewa na mrija wa chakula, hali ambayo inaweza kusababisha:

1. Shida katika kupumua

2. Kikohozi

3. Sauti kuwa ya mikwaruzo

4. Shida wakati wa kumeza chakula

5. Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono juu

6. Mtu kupatwa na tatizo la misuli ya shingo kukaza sana

MADHARA YA GOITA AU ROVU NI YAPI?

1. Shida wakati wa kumeza au kupumua

2. Kiwango cha chini cha homoni za thyroid (Hypothyroidism)

3. Kiwango cha juu cha homoni za thyroid (Hyperthyroidism)

4. Saratani ya tezi ya thyroid (thyroid cancer)

5. Goita yenye vivimbe inayozalisha homoni kwa wingi (toxic nodular goiter)

•Soma: Ugonjwa wa Mgongo Wazi kwa Watoto,chanzo,Dalili na Tiba yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Karibu Sana..!!!

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!