Ugonjwa wa Stiff Person Syndrome,Chanzo,Dalili na Tiba

 Ugonjwa wa Stiff Person Syndrome,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa Kukakamaa Misuli(Stiff person syndrome) ni Ugonjwa ambao ni nadra Sana kutokea yaani huweza kutokea kwa Mtu Moja kati ya watu Million Moja,

na ugonjwa huu upo kwenye kundi la Rare neurological disorder, ambapo huathiri mfumo mkuu wa fahamu(central nervous system) Hapa tunazungumzia Ubongo pamoja na Uti wa Mgongo.

Watu wenye Ugonjwa huu mara nyingi hupatwa na tatizo la Misuli kukakamaa na kukaza kwenye maeneo mbali mbali Mwilini ikianzia kwenye Kiwiliwili, na baadae kwenye maeneo kama vile Miguuni,mikononi,Usoni n.k

Ukakamavu huu wa Misuli huenda Sambamba na maumivu makali ya Misuli yaani Painful muscle spasms,

Kama nilivyosema hapo Awali,,Ugonjwa huu wa Stiff Person Syndrome ni Nidra Sana kutokea, huweza Kutokea Kwa Mtu Mmoja kati ya Watu Million Moja,

Na Tafiti zinaonyesha,Huwapata wanawake zaidi ya wanaume, yaani hatari ya kutokea kwa Wanawake ni Mara mbili zaidi ya Kwa wanaume.

Hatari ya Ugonjwa huu kutokea ni kubwa kwa watu wenye matatizo mengine kama vile;

- Magonjwa ya Mfumo wa Kinga Mwili yaani Autoimmune disorders

• Ugonjwa wa kisukari diabetes,

• Tatizo la thyroiditis,

• Ugonjwa wa vitiligo

• Tatizo la Damu kupungua yaani pernicious anemia.

- Pia kwa watu wenye Saratani mbali mbali kama vile;

• Saratani ya Matiti

• Saratani ya Mapafu

• Saratani ya Tezi la Thyroid

• Saratani ya Utumbo mpana

• Pamoja na Hodgkin’s lymphoma.

DALILI ZA UGONJWA HUU WA STIFF PERSON SYNDROME

Dalili zake huweza kutokea kwenye Umri wowote,ila Mara nyingi ni Kuanzia watu wenye Miaka 30 Mpaka 60,

Na dalili zake huweza kuchukua miezi kadhaa mpaka miaka kadhaa kuanza kuonekana toka mtu kupatwa na tatizo hili.

Dalili zake ni Pamoja na;

- Misuli kuanza kukakamaa,Kukaza na kuongezeka ukubwa kwenye maeneo kama vile tumboni,miguuni, mikononi n.k

Hali hii mara nyingi huanzia kwenye eneo la Kiwiliwili ndipo baadae maeneo mengine ya Mwili,

- Kupata maumivu makali kwenye Misuli pamoja na hali ya kuwaka Moto

Tatizo hili huweza kusababisha hata Mtu kushindwa kutembea kutoka sehemu Moja kwenda nyingine, hasa pale ambapo Misuli ya Miguuni huathiriwa zaidi.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA STIFF PERSON SYNDROME

Hakuna Sababu Halisi au ya moja kwa moja ambayo inahusishwa na tatizo hili, Ila watafiti mbali mbali wameonyesha uhusiano wa karibu kati ya Ugonjwa huu Pamoja na;

Matatizo kwenye mfumo wa Kinga Mwili(autoimmune disorder), ambapo Mfumo wako wa Kinga Mwili huanza mashambulizi dhidi ya Seli ambazo hazina tatizo lolote(healthy cells).

VIPIMO HIVI HUWEZA KUTUMIKA KUGUNDUA UGONJWA HUU

• Kipimo cha Damu yaani Blood test

• Lumbar puncture (spinal tap):

• Electromyography (EMG) n.k

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA STIFF PERSON SYNDROME

matibabu ya Ugonjwa huu yapo kwenye kudhibiti Dalili tu zinazotokana na Ugonjwa huu, Ila Mpaka Sasa hakuna Tiba ya Moja kwa Moja ili Kuondoa Kabsa Ugonjwa huu,

Kulingana na Dalili zake, Dawa kama vile; Jamii ya benzodiazepines Mfano; diazepam na clonazepam

au baclofen huweza kutumika kutibu Misuli inayokakamaa na Kukaza.

Matibabu mengine ni kama vile; intravenous immunoglobulin (IVIG), plasmapheresis, rituximab, au Huduma ya autologous stem cell transplant.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!