Tatizo la Gastroparesis,chanzo,dalili pamoja na Madhara yake
Gastroparesis ni hali ambayo huathiri harakati ya kawaida ya hiari ya misuli (motility) kwenye tumbo lako. Kwa kawaida, mikazo yenye nguvu ya misuli husukuma chakula kupitia njia yako ya usagaji chakula.
Lakini ikiwa una gastroparesis, motility ya tumbo lako hupunguzwa au haifanyi kazi kabisa,Hali hii huzuia tumbo lako kutoa products zilizopo ndani,
Sababu ya moja kwa moja inayopelekea tatizo la gastroparesis haijulikani,Wakati mwingine huhusishwa na shida nyingine kama vile ugonjwa wa kisukari, na watu wengine hupata gastroparesis baada ya upasuaji.
Dawa fulani, kama vile dawa za kupunguza maumivu aina ya opioid, baadhi ya dawa za kutibu tatizo la mfadhaiko(stress), na shinikizo la damu na dawa za mzio(allergies), zinaweza kusababisha kupungua kwa tumbo na kusababisha dalili zinazofanana na tatizo hili. Kwa watu ambao tayari wana gastroparesis, dawa hizi zinaweza kufanya hali yao kuwa mbaya zaidi.
Dalili za Tatizo la Gastroparesis
Tatizo la Gastroparesis linaweza kuingilia mfumo wa kawaida wa umeng'enyaji chakula, kisha kupelekea dalili mbali mbali ikiwemo; Hali ya kichefuchefu,kutapika, pamoja na maumivu ya tumbo.
Pia Tatizo la Gastroparesis linaweza kusababisha matatizo zaidi kwa mtu mwenye ugonjwa wa kisukari. Ingawa
Tatizo la Gastroparesis halina Tiba kabsa, kubadilisha mfumo wa maisha ikiwemo chakula,pamoja na matumizi ya dawa huweza kusaidia kudhibiti dalili zinazotokana na tatizo hili.
Dalili za Tatizo la Gastroparesis ni pamoja na;
- Kutapika
- Kuhisi kichefuchefu
- Tumbo kujaa gesi au kuvimbiwa
- Maumivu ya Tumbo
- Kutapika chakula kama kilivyo,muda mfupi baada ya kula
- Kupata tatizo la Tindikali kupanda(acid reflux)
- Kubalika kwa kiwango cha sukari kwenye damu
- Kukosa hamu ya kula
- Kupungua kwa Uzito wa mwili
Chanzo cha Tatizo la Gastroparesis
Mpaka sasa chanzo halisi cha Tatizo la Gastroparesis hakifahamiki, Lakini kwa baadhi ya Kesi(Cases), Tatizo la Gastroparesis husababishwa na uharibifu wa neva ikiwemo neva zinazodhibiti tumbo lako, kwa kitaalam hujulikana kama vagus nerve.
Vitu ambavyo huongeza hatari ya Mtu kupata Tatizo la Gastroparesis ni pamoja na;
1. Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari
2. kuwahi kufanyiwa upasuaji wa tumbo au umio(Abdominal or esophageal surgery)
3. Kupata maambukizi ya Virusi
4. Matumizi ya baadhi ya dawa,ikiwemo dawa za maumivu jamii ya narcotic(narcotic pain medications)
5. Kuwa na matatizo ya kiafya ikiwemo Scleroderma(a connective tissue disease)
6. Kuwa na magonjwa yanayoathiri kwenye mfumo wa fahamu(Nervous system diseases) kama vile ugonjwa wa Parkinson's disease au multiple sclerosis.
7. Kuwa na tatizo la Underactive thyroid (hypothyroidism)
8. Pia wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Tatizo la Gastroparesis kuliko wanaume.
Madhara ya Tatizo la Gastroparesis
Madhara ya Tatizo la Gastroparesis ni pamoja na;
- Upungufu mkubwa wa maji mwilini, hasa kutokana na kutapika sana
- Kuwa na tatizo la Utapiamlo(Malnutrition).
Kukosa hamu ya kula kunaweza kusababisha mwili kukosa kalori za kutosha, au wakati mwingine mwili huwezi kunyonya virutubisho vya kutosha kwa sababu ya kutapika.
- Chakula ambacho hakijameng'enywa kubaki tumboni na kutengeneza kitu kigumu kinachojulikana kama bezoar. Bezoars huweza kusababisha kuhisi kichefuchefu na kutapika zaidi, na pia huweza kuhatarisha maisha zaidi kwani huweza kuzuia chakula kupita kwenye utumbo mdogo.
Hayo ndyo baadhi ya Madhara ya Tatizo la Gastroparesis
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!