Dawa ya Kutibu Kisonono Kabsa,Wengi Mnaita Gono
Je, ni Ipi dawa sahihi ya kutibu Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?
Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,
Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;
Dalili za Ugonjwa wa Kisonono au Gono
DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;
- Kutokwa na usaha kwenye Uume
- Uchafu wa majimaji meupe, ya njano, au ya kijani kutoka kwenye uume.
- Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita
- Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation
- Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko
- Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu
- Kupata maumivu kwenye korodani.
- Kupata Maumivu au uvimbe katika sehemu ya haja kubwa (ikiwa maambukizi yameathiri eneo hilo).
- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa n.k.
Dawa ya Kutibu Kisonono
Dawa za kisonono au Gono huweza kutibu kabsa tatizo hili likaisha ikiwa umepata tiba Sahihi na hujakutana na mazingira hatarishi ya kupata maambukizi haya tena baada ya Tiba.
Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati wa Kutumia Dawa za kutibu kisonono kwani badala ya kutibu Kisonono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”
Kwa hivi Sasa,Ukinzani huu kwenye Ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio Ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Ngumu kuipata.
Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kugundulika una ugonjwa wa Kisonono, hakikisha unapata dawa ya Kisonono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.
Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Kisonono – ufuatiliaji wa dawa ya Kisonono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.
Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,
Kuhusu Kipindi cha Matibabu:
Wagonjwa wanaotibiwa maambukizi ya koo wanashauriwa kufanyiwa kipimo cha uhakiki wa tiba (test of cure) siku 7–14 baada ya matibabu, kwa sababu koo ni eneo gumu zaidi kuponya maambukizi.
Kwa wagonjwa wengine (wasio na maambukizi ya koo), matibabu kwa dozi moja ya sindano mara nyingi hutosha, na hakuna haja ya kipimo cha uhakiki wa tiba isipokuwa dalili zitaendelea au maambukizi yawe sugu.
wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.
Dawa ya gono;
Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”
Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ambapo huweza kutumika ni pamoja na;
- Sindano
- Na Vidonge
Ingawa dawa hizi Zitazuia maambukizi ya Gono hazitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.
NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.
NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!