Magonjwa ya Zinaa na dalili zake

Magonjwa ya Zinaa na dalili zake

Magonjwa ya Zinaa ni yale magonjwa yote ambayo huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa Mtu mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Magonjwa hayo husababishwa na maambukizi ya Viini mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Parasite au Virusi

Kuna Magonjwa Mengi ya Zinaa ila katika Makala hii ntaeleza Magonjwa Makuu Manne(4);

  1. Ugonjwa wa Kisonono
  2. Ugonjwa wa Kaswende
  3. Ugonjwa wa Chlamydia
  4. Pamoja na Trichomoniasis

1. Ugonjwa wa Kisonono

Ugonjwa wa Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na Bacteria ambaye kwa kitaalam hujulikana kama Neisseria gonorrhoeae, Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

Zipo Dalili mbali mbali za Ugonjwa huu wa Kisonono ikiwemo;
  • Mwanaume Kutokwa na usaha sehemu za Siri,kwenye uume
  • Mwanamke kutokwa na ute ute ambayo umechanganyika na usaha ukeni n.k

2. Ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa ambapo Chanzo chake ni maambukizi ya bakteria aitwaye Treponema pallidum,

Bakteria hawa huingia mwilini kupitia mikato,michubuko au mikwaruzo kwenye ngozi,kidonda au kupitia utando wa ndani wenye unyevunyevu au maji maji n.k.

Zipo Dalili mbali mbali za Ugonjwa wa Kaswende ambazo zimegawanyika kulingana na hatua au Stage ya Ugonjwa huu;

Ugonjwa wa kaswende umegawanyika kwenye hatua kuu Nne yaani; 

  • primary,
  • secondary,
  • latent/hidden
  • Pamoja na tertiary,

Kwenye hatua mbili za mwanzo(primary na secondary) kaswende huambukiza zaidi, kwenye hidden au latent stage kaswende hubaki kuwa active lakini mgonjwa anaweza asionyeshe dalili zozote, na kwenye Tertiary Stage hapa ugonjwa huleta madhara zaidi kwenye afya.

(1).Primary syphilis

Hapa huhusisha wiki 3 mpaka 4 toka Mgonjwa kuambukizwa bacteria wanaosababisha Kaswende,Na dalili zinazoanza kuonekana ni kama kidonda kidogo sana ambacho hata hakina maumivu yoyote kwa kitaalam huitwa chancre,

Kidonda hiki kidogo hakina maumivu yoyote ila kinakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuambukiza, Mtu anaweza hata asijue kwamba ana kijidonda hiki(chancre),

Na kinatokea sehemu ambapo bacteria wemeingilia Mwilini kama vile Mdomoni,Sehemu za Siri au kwenye njia ya haja kubwa.

Wastani kidonda huweza kuonekana wiki 3 baada ya kuambukizwa, lakini huweza kuchukua siku 10 mpaka 90 kuonekana, na Wakati mwingine Mtu huweza kuwa na dalili Moja tu ya Kuvimba kwa tezi za Lymph( yaani Swollen lymph nodes).

Na mtu mwingine huweza kuambukizwa kwa kugusana na kijidonda hicho(Direct contact) hasa wakati wa kufanya mapenzi.

(2).Secondary syphilis

Katika hatua hii Ngozi inaweza kuwa na vipele au Rashes, ambavyo huacha vimadoa doa au alama kwenye ngozi,maumivu ya koo au mtu kuwa na sore throat,n.k

Rashes hizi kwenye ngozi haziwashi na mara nyingi huonekana kwenye viganja vya mikono pamoja na kwenye miguu kwa chini(sole), japo pia zinaweza kuonekana maeneo mengine.

Na watu wengine wanaweza wasijue mpaka zinaisha zenyewe.

Dalili zingine kwenye secondary syphilis ni pamoja na;

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuvimba kwa lymph nodes

- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

- Kupata Homa

- Uzito wa mwili kushuka au kupungua

- Nywele kunyonyoka(hair loss)

- Maumivu kwenye joints n.k

KUMBUKA;Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa makini kwa Mgonjwa mwenye shida hii,maana tafiti nyingi zinaonyesha ugonjwa wa kaswende unaweza kuwa na dalili ambazo hufanana kabsa na magonjwa mengine au Nonspecific symptoms, hali ambayo inaweza kuwa ngumu hata mtu kujua kama ana tatizo hili.

(3).Latent syphilis

Hatua ya tatu ya ugonjwa wa kaswende inajulikana kama latent au hidden, stage.

Dalili zote zilizoonekana kwenye hatua ya kwanza na ya pili zinapotea, hivo hakuna dalili yoyote inaonekana kwenye stage hii ndyo maana ya kupewa jina la hidden au latent stage.

Japokuwa dalili zimepotea ila Bacteria bado wapo mwilini na wakati mwingine huweza kuchukua muda kabla ya kwenda stage ya nne(tertiary stage of syphilis).

(4).Tertiary syphilis

Baadhi ya tafiti zinaonyesha ni asilimia 14% mpaka 40% ya watu wenye ugonjwa wa kaswende hufika stage hii,

Hatua hii ya ugonjwa wa kaswende inaweza kuchukua Muda mrefu sana hata miaka mpaka mtu kuingia kwenye stage hii toka siku ya kwanza ya maambukizi(initial infection).

Na madhara yake kwenye stage hii ni makubwa sana hata kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

3. Ugonjwa wa Chlamydia

Chlamydia ni Ugonjwa wa Zinaa ambao husababishwa na kuenezwa na bakteria aitwaye Chlamydia trachomatis, na unaweza kuambukizwa kwa njia ya kufanya tendo la ndoa.

Dalili za Ugonjwa wa Chlamydia ni pamoja na:

  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na Uchafu ukeni
  • Kutokwa na Uchafu kwenye Uume
  • Kupata maumivu ukeni wakati wa tendo
  • Kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuvuja damu ukeni baada ya tendo
  • Kupata maumivu ya Korodani n.k

Kumbuka; Dalili hizi pia huweza kuingiliana na magonjwa mengine.

 4. Trichomoniasis

Ugonjwa huu wa Trikomonasi hutokana na mtu kupata maambukizi ya vimelea aina ya PROTOZOA vinavyojulikana kwa jina la TRICHOMONAS VAGINALIS ambavyo pia huweza kuvipata kwa njia ya kujamiiana.

DALILI ZA UGONJWA WA TRIKOMONASI NI PAMOJA NA HIZI;

(a) Kwa Wanawake

1. Mgonjwa kupata miwasho sehemu za siri, ambapo hupata miwasho maeneo ya kuzunguka ukeni ikiwemo pamoja na ngozi ya mashavu ya uke.

2. Kutokwa na uchafu sehemu za siri  wenye rangi kama njano,nyeupe au Kijani kwa mwanamke

3. Mwanamke kuvuja damu sehemu za siri

4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu pamoja na kuvimba

5. Kuhisi hali kama ya kuungua sehemu za siri mara kwa mara

6. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

7.Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa

8. Kupata hisia za mkojo mara kwa mara ndani ya mda mfupi n.k.

(b). Kwa Wanaume

1. Mgonjwa kupata miwasho sana sehemu za siri, kwenye Njia ya Mkojo ikiwemo eneo la kitundu kidogo cha mkojo kwenye uume

2. Kutokwa na uchafu kwenye Njia ya mkojo

3. Kuhisi hali ya kuchomwa au kuungua baada ya mwanaume kutoa mbegu za kiume au baada ya mwanaume kumwaga shahawa akifanya mapenzi

4. Kuhisi hali ya kuungua au kuchomwa wakati wa kukojoa

5. Kupata hisia za kukojoa mara kwa mara ndani ya mda mfupi n.k.

Kumbuka; Dalili hizi pia huweza kuingiliana na magonjwa mengine.

Je,Una Matatizo haya na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!